Apigwa risasi akiingia Ikulu

Apigwa risasi akiingia Ikulu

11 June 2019 Tuesday 17:02
Apigwa risasi akiingia Ikulu

Nairobi, Kenya

MWANAFU NZI wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, anauguza majeraha katika katika Hospitali ya taifa ya Kenyatta baada ya kupigwa risasi na polisi kwa kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikwea lango moja la Ikulu, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na maafisa wa polisi wanaolinda kwenye lango hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.  Siku ya Jumapili Jioni Kibet aliandika katika mtandao wake wa Facebook kuwa ataingia Ikulu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena-Mararo Kisa hicho kilitokea Jumatatu na mshukiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa na kusajiliwa katika Kitabu cha Matukio nambari 39 kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu.

''Tunachukua fursa hii kukumbusha umma kwamba Ikulu ni mahali polipotengwa kuwa chini ya ulinzi mkali kwa mujibu wa Sheria ya Maeneo Yanayolindwa (Protected Areas Act). Kwa sababu hiyo, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia Ikulu pasipo na ruhusa ya mamlaka yenye jukumu hilo.'' alisema Bi Kanze.

Ameongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini nia yake ya mshukiwa huyo kuingia Ikulu kinyume cha sheria na hatua zifaazo zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Kisa hicho kimezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini Kenya huku baadhi watu wakihoji kwanini mwanafunzi huyo aliamua kuchukua hatua hiyo.

BBC

Updated: 11.06.2019 17:14
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.