AU yaisimamisha Sudan

AU yaisimamisha Sudan

06 June 2019 Thursday 19:39
AU yaisimamisha Sudan


TUME ya amani na usalama katika muungano wa nchi za Afrika (AU) umesimamisha shughuli zote za Sudan ndani ya umoja huo.

Imechukua  uamuzi huo kufuatia mauaji ya raia wasio na hatia nchini Sudan katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

Muungano huo umetaka uchunguzi kufanywa kuhusu mauaji hayo ambayo yanadaiwa kutekelezwa na vikosi vya usalama.

Tume hiyo inasema kuwa marufuku hiyo ilikubaliwa na wanachama na itaanza kutekelezwa mara moja.

Vilevile imetishia kuchukua hatua dhidi ya watu binafsi katika baraza hilo la mpito iwapo jeshi litakataa kukabidhi mamlaka kwa raia.

Maamuzi hayo yaliafikiwa baada ya kikao cha dharura kilichofanyika kwa takriban saa tano.

Hatua hiyo inajiri huku waziri wa afya nchini Sudan akisema kuwa ni watu 46 pekee waliofariki katika ghasia za hivi majuzi madai yanayopingwa na kamati ya madaktari nchini humo ambao wamesema kuwa idadi hiyo inafika watu zaidi ya 100.  Hali ya wasiwasi imepanda nchini humo tangu Jumatatu wakati ambapo vikosi vya usalama vilianzisha msako dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia.

Kikosi cha kijeshi cha RPS kilichoshutumiwa kwa kutekeleza mauaji hayo kimekuwa kikipiga doria katika mji mkuu wa Khartoum.

Muungano wa Afrika umeipiga marufuku Sudan kushiriki katika shughuli zozote za Muugano huo hadi taifa hilo litakapounda serikali ya mpito inayoongozwa na raia.

Uamuzi huo unajiri baada muungano huo kuwapatia watawala wa kijeshi wa taifa hilo siku 60 kukabidhi mamlaka kwa raia la sivyo wapigwe marufuku.

Updated: 06.06.2019 19:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.