Baraza la kijeshi, waandamanaji wafikia muafaka 

Baraza la kijeshi, waandamanaji wafikia muafaka 

05 July 2019 Friday 11:06
Baraza la kijeshi, waandamanaji wafikia muafaka 

Khartoum, Sudan
Baraza tawala la kijeshi nchini Sudan na vuguvugu la maandamano wamekubaliana kuhusu masharti ya kuundwa kwa serikali ya pamoja. 

Pande hizo mbili zimekubaliana kuunda baraza la serikali ya juu, ambayo itaongozwa kwa kubadilishana kati ya jeshi la raia. 

Kwa ujumla, awamu ya mpito imepangwa kudumu kwa karibu miaka mitatu, wakati ambapo uchaguzi mkuu utaitishwa, amesema mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Mohamed El-Hacen Lebatt. 

Awali, baraza la kijeshi lilitekeleza sharti la kuwaachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa kama ilivyodaiwa na upinzani, ambapo wapiganaji 235 wa kundi la waasi la "jeshi la ukombozi wa Sudan" waliachiwa kutoka gerezani.

DW

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.