Jeshi la Sudan lasaini makubaliano ya kugawana uongozi na wapinzani

Jeshi la Sudan lasaini makubaliano ya kugawana uongozi na wapinzani

17 July 2019 Wednesday 11:43
Jeshi la Sudan lasaini makubaliano ya kugawana uongozi na wapinzani

Khartoum, Sudan
JESHI la Sudan limesaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani.

Baraza tawala la kijeshi na viongozi wa upinzani nchini Sudan, wamesaini makubaliano ya kugawanya uongozi baada ya mazungumzo ya usiku kucha kumaliza mzozo nchini humo.

Kumefanyika sherehe zilizomalizika hivi punde katika hoteli ya Corinthia katika mji mkuu wa Khartoum. Makubaliano hayo yanatazamia miaka mitatu ya uongozi wa pamoja utakaofuatwa kwa uchaguzi mkuu.

Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, viongozi wa pande zote wamezungumzia kizazi kipya katika taifa ambalo limeshuhudia ghasia na mauaji ya mamia ya waandamanaji tangu kutimuliwa kwa kiongozi aliyekuwepo Omar Al Bashir mnamo April, 2019 .

Updated: 17.07.2019 11:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.