Jeshi laingia mtaani kudhibiti mauaji na uhalifu

Jeshi laingia mtaani kudhibiti mauaji na uhalifu

19 July 2019 Friday 10:02
Jeshi laingia mtaani kudhibiti mauaji na uhalifu

Capetown, Afrika Kusini
WANAJESHI nchini Afrika Kusini wanafanya doria kwenye mitaa ya viunga kadhaa vya mji wa Cape town, ambavyo vimekuwa vikikumbwa na vurugu za magenge ya watu.

Hatua hiyo inafuatia baada ya watu zaidi ya 40 kuuwawa mwishoni mwa wiki iliyopita. Pia  hatua hiyo  imelenga kusaidia polisi kupambana dhidi ya wimbi la ongezeko la vitendo vya mauaji.

Wanajeshi wenye silaha waliwasili na magari yao ya kijeshi siku ya Alhamisi Julai 18, 2019 na kuanza kufanya operesheni ya ukaguzi katika eneo la Manenberg, eneo linadaiwa kushamiri kwa ghasia.

Vikosi vya kijeshi vitapelekwa kwenye maeneo 10 ya mji wa Cape town. 

Takwimu kutoka kwenye nyumba za kuhifadhia miili zinaonyesha ongezeko la vifo katika eneo hilo, huku kukiwa na ripoti ya vifo vya watu 1,000 mwaka huu pekee.

Mwezi uliopita, askari sita waliokuwa kwenye kikosi cha kupambana na magenge yanayofanya vurugu walijeruhiwa vibaya wakiwa kwenye doria.

Hii si mara ya kwanza vikosi vya kutuliza ghasia vinaingia mtaani. Miaka minne iliyopita, Jeshi, likiwa limeambatana na polisi na idara nyingine za serikali katika operesheni ya kupambana na uhalifu.

Lakini wakosoaji wa mambo wanasema jeshi si suluhu ya ghasia zinazokumba maeneo kadhaa ya Cape town kwa miaka kadhaa sasa.

PICHANI; Wanajeshi wakiwa kwenye doria mjini Capetown

Updated: 19.07.2019 10:18
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.