Kaburi la Etienne Tshisekedi lagharimu Bilioni 5.7 kuzikwa leo

Kaburi la Etienne Tshisekedi lagharimu Bilioni 5.7 kuzikwa leo

31 May 2019 Friday 09:42
Kaburi la  Etienne Tshisekedi lagharimu Bilioni 5.7 kuzikwa leo

KABURI atakalozikwa  kiongozi wa upinzani ambaye pia ni baba wa  rais wa DR Congo, Etienne Tshisekedi litagharimu fedha za kimarekani  takriban dola milioni 2.5 sawa na fedha za  kitanzania  takriban bilioni 5.7.

Taarifa ya familia yake inaeleza  kiongozi huyo atazikwa Jumamosi ya Juni 1, 2019 jijini Kinshasa na shughuli za kuuaga mwili  zinaendelea leo katika uwanja wa taifa wa mpira wa nchi hiyo kwa 'wacongo man' kutoa salam zao za mwisho. Jioni atafanyiwa misa itakayoongozwa kiongozi mkuu wa dhehebu Romani Katholiki nchini DRC Congo

Atazikwa katika uwanja wa Martyrs Stadium, Uwanja huo wa Martyrs unabeba zaidi ya raia 80.

Mwili wa kiongozi huyo uliwasili jana jioni Mei 30,2019  ikiwa ni miaka miwili baada ya kifo chake nchini Ubelgiji. 

Takriban Marais watano wanatarajia kuhudhuria maziko ya kiongozi huyo.

Alifariki mjini Brussels akiwa na umri wa miaka 84 mnamo mwezi februari 2017 lakini mwili wake ulisalia katika mji huo wa Ubelgiji kutokana na wasiwasi wa kisiasa na utawala wa rais wa zamani wa taifa hilo Josep kabila.

Kulingana na nduguye Askofu Gerard Mulumba amesema tayari maandalizi katika uwanja huo ikiwezmo ujenzi wa jukwaa umekamilika mbali na yale ya maafisa wa polisi ambao wataongoza gwaride ili kumpatia heshima za mwisho baba huyo wa upinzani.

Atazikwa kama shujaa.

AKIWA mwanasiasa wa muda mrefu, Etienne Tshisekedi alihudumu katika upinzani kwa miongo kadhaa lakini hakufanikiwa kuiongoza nchi hiyo.

Akiwa mkosoaji mkubwa wa aliyekuwa dikteta Mobutu Sese Seko, alianzisha chama cha Union for Democracy and Special Progress UDPS mwaka 1982 baada ya kuhudumia kifungo jela.

Mwaka 1997, baada ya Mobutu kung'atuliwa madarakani na kundi lililoongozwa na Kabila, Tshisekedi alianza kuwa mpinzani wa utawala mpya , msimamo aliokuwa nao hata baada ya mauaji ya Laurent 2001 huku mwanawe akipanda katika hatamu za uongozi.

Baada ya kushindwa katika uchuzi wa 2011 uliodaiwa kukumbwa na udanganyifu mkubwa , Tshisekedi alikataa kutambua utawala wa Kabila hadi kifo chake.

Yapata miaka miwili baada ya kifo chake , mnamo mwezi Januari 24, mwanawe Felix Tshisekedi aliapishwa kuwa rais baada ya uchaguzi ambao ulimfanya Kabila kuondoka madarakani baada ya miaka 18.

Uchaguzi huo hata hivyo ulikumbwa na madai mengi ya udanganyifu huku siasa za taifa hilo bado zikitawaliwa na Kabila ambaye alijipatia umaarufu mkubwa akiwa madarakani.

Siku ya Jumatatu Tshisekedi alimteua mwanasiasa wa muda mrefu Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa waziri mkuu.

Updated: 01.06.2019 08:46
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.