Maafisa nane wa jeshi kushtakiwa

Maafisa nane wa jeshi kushtakiwa

28 July 2019 Sunday 07:47
Maafisa nane wa jeshi kushtakiwa

Khartoum, Sudan
MAAFISA  nane wa jeshi nchini Sudan watashtakiwa  kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, wakidaiwa kushiriki vitendo vya mauaji ya waandamanaji  Juni 3, 2019.

Waendesha mashtaka wa serikali walitangaza hatua hiyo baada ya kufanyia uchunguzi vitendo vya mauaji, baada ya takribani watu 87 kupoteza maisha mjini Khartoum.

Wanaharakati wapinzani wanasema kuwa idadi ya waliopoteza maisha inakaribia 130.

Waandamanaji waliuawa mwezi Juni baada ya vikosi vya usalama kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakilitaka jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Kwa sheria ya kijeshi ya Sudan, hukumu ya uhalifu dhidi ya binaadamu ni adhabu ya kifo. Fath al -Rahman Saeed, alikuwa kiongozi wa kamati aliyeteuliwa kuchunguza vitendo vya mauaji, hakutaja majina ya maafisa wanaoshutumiwa kutekeleza vitendo hivyo.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa watatu walikiuka amri kwa kupeleka vikosi vya usalama kwenye eneo ambalo waandamanaji walikuwa wamepiga kambi nje ya jengo la wizara ya ulinzi.

Vikosi vya usalama ''vilivunja sheria na kuingia kwenye eneo hilo'', alinukuliwa na shirika la habari la Ufaransa akisema ''Waliondoa vizuizi, wakafyatua gesi ya kutoa machozi kisha kufyatua risasi hovyo hovyo na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, pia maturubai yao yaliungua moto.''

Mwenyekiti wa kamati pia ametetea uamuzi wa kusambarataisha makundi ya watu kwenye eneo jingine akisema: ''Baadhi ya watu waliunda mkusanyiko kwa ajili ya kutekeleza vitendo vya uvunjaji sheria.

''Hali hiyo ilisababisha tishio la kiusalama, hali iliyolazimu mamlaka kuchukua hatua.''Idadi ya waliopoteza maisha imedaiwa kuwa 87 huku wengine 168 walijeruhiwa.

Kulikuwa na hali ya taharuki miongoni mwa wapinzani, ambao walikuwa wamepiga kambi nje kwa miezi kadhaa na maandamano yaliyomuondoa madarakani rais Omar al- Bashir mwezi Aprili

Hata hivyo, maelfu ya waandamanaji walirejea mitaani majuma machache baadae baada ya kung'oka kwa utawala wa Bashir. Maandamano hayo makubwa yaliwafanya majenerali kurejea mazungumzo kuhusu kugawana madaraka. Hatimaye pande mbili zilikubaliana.

Updated: 28.07.2019 08:06
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.