Mahakama yampiga faini rais mstaafu

"Moi alinyakua ardhi hiyo kinyume cha sheria miaka 36 iliyopita, lakini ilisajiliwa kwa jina la Moi mwaka 2007"

Mahakama yampiga faini rais mstaafu

"Moi alinyakua ardhi hiyo kinyume cha sheria miaka 36 iliyopita, lakini ilisajiliwa kwa jina la Moi mwaka 2007"

18 May 2019 Saturday 07:14
Mahakama yampiga faini  rais mstaafu

Na mwandishi wetu, Nairobi

MAHAKAMA  nchini Kenya imemuamuru rais wa zamani wa Kenya,  Daniel  Arap Moi kulipa fidia ya dola milioni 1.06 kwa mjane ambaye alimchukulia ardhi yake kenyume cha sheria

 Moi alinyakua ardhi ya heka 53 iliyokuwa mali ya mjane Susan Cheburet Chelugui, alisema Jaji Anthony Ombwayoji na kwamba Moi alinyakua ardhi hiyo kinyume cha sheria miaka 36 iliyopita, lakini ilisajiliwa kwa jina la  Moi mwaka 2007.

Mume wake Chelugui Noah Chelugui alikuwa chifu wakati wa utawala wa Moi.

Rais huyo wa zamani ambaye ndiye rais aliyekuwa mamlakani kwa muda mrefu zaidi , alishutumiwa na Bi Chelugui na mtoto wake wa kiume David Chelugui kwa kusajili ardhi ya familia yao kwa jina lake miaka miwili baada ya mume wa Bi Chelugui kufariki dunia.

Inasemekana baadae  Moi aliiuza ardhi hiyo kwa kampuni ya utengenezaji wa mbao Plywood Limited.

Kampuni ya Rai Plywood Limited iliwaeleza majaji kuwa ilinunua ardhi hiyo kutoka kwa Moi mnamo mwaka 2007 baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa kisheria kuhusu ardhi hiyo.

Hata hivyo,  Moi hakuweza kuipatia mahakama ushahidi wowote juu ya jinsi alivyopata ardhi.

Jaji Anthony Ombwayo alisema  Moi alikuwa na mienendo ya "isiyo ya kawaida, ukiukaji katiba, kutofuata utaratibu " na "yenye dosari ".  Moi alikuwa rais wa pili wa Kenya mwaka 1978 ambapo alihudumu hadi mwaka 2002. Katika utawala wake   alishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Kutokana na shinikizo la kimataifa, aliruhusu uchaguzi wa vyama vingi mnamo mwaka 1992 ,uliotawaliwa na ghasia zilizosambaa nchini na madai ya wizi wa kura.

Wengi wanamatumaini kuwa hukumu hii dhidi ya  Moi itaonekana kama jaribio na kwamba itatuma ujumbe kwa watu kwamba hawawezi tu kuwa wananyakua ardhi tena za watu maskini.

Updated: 18.05.2019 07:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.