Mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Saudia Arabia kuhiji

Mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Saudia Arabia kuhiji

27 July 2019 Saturday 07:33
Mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Saudia Arabia kuhiji


WIZARA ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imeeleza kuwa mwaka huu haitatoa viza ya kusafiria kwa mahujaji kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC)

Wizara imesema uamuzi ulifikiwa kutokana na uamuzi wa shirika la afya duniani, WHO kutangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC ni suala la dharura inayohitaji kushughulikiwa na jumuia ya kimataifa.

''Mpango wa kutoa viza kwa watu wanaoingia kutoka DRC umesimamishwa, kwa ajili ya usalama wa mahujaji,'' wizara.

Saudi Arabia awali ilisema takribani watu 410 kutoka nchini DRC wanatarajia kwenda kuhiji mjini Makka baadae mwezi huu, alisema Kiongozi wa kiislamu nchini DRC, Imamu Djuma Twaha.

''Kuna watu walikuwa wamejiandaa kwa miaka mingi, wakati mwingine miaka kumi wakijichanga kiasi cha pauni 3,400 kwa ajili ya kufanya safari kwa ajili ya hija,'' alieleza.

WHO ilitangaza hali ya dharura kutokana na mlipuko wa Ebola  Julai 17, lakini imezitaka nchi kutofunga mipaka yao dhidi ya watu wanaofanya safari au biashara.

Mlipuko wa Ebola ni ugonjwa wa pili kwa ukubwa katika historia ya nchi hiyo, ulianza mwezi Agosti  mwaka jana na unaathiri majimbo mawili ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Zaidi ya watu 2500 wameathiriwa na ugonjwa huo na theluthi mbili kati yao wamepoteza maisha.

Ilichukua siku 224 kwa idadi ya walioathirika kufika 1,000 , lakini ndani ya siku 71 zaidi idadi ilifika 2,000.

Watu takribani 12 huripotiwa kupata ugonjwa huo kila siku.

Kwanini ugonjwa huu haujadhibitiwa?
Wafanyakazi wa afya wamekua wakipata vikwazo vya kutoaminika na pia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Watu wengine hawawaamini watoa huduma za afya, hivyo hufanya watu wenye dalili za ugonjwa huo kukwepa matibabu, hali hii inawia vigumu kuzuia kuenea kwa virusi vya ebola.

Ingawa zaidi ya watu 1,300 wamepoteza maisha tangu mwezi Agosti, Shirika la misaada la Oxfam linasema linakutana na watu kila siku ambao hawaamini kama kuna virusi vya ebola.

Tangu mwezi Januari kulikua na matukio 198 ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, na kusababisha majeruhi 58.

BBC

Updated: 27.07.2019 07:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.