Mashia wapigwa marufuku Nigeria

Mashia wapigwa marufuku Nigeria

05 August 2019 Monday 14:53
Mashia wapigwa marufuku Nigeria

Abuja, Nigeria
Serikali ya Nigeria imepiga marufuku Waislam wa dhehebu la Shia wanaoungwa mkono na Iran, kwa madai ya kusababisha vurugu nchini humo na kulitaja kuwa ''adui wa taifa''

Vugu vugu la Waislamu nchini Nigeria (IMN) linapinga marufuku hiyo likisema linaendesha shughuli zake kwa amani na kwamba serikali imekuwa ikipanga njama dhidi yake.

Hatua hiyo imesababisha hali ya taharuki na hofu ya kuzuka kwa mzozo kati ya Waislamu wa Kishia na Wasunni katika taifa hilo la Afrika lenye utajiri wa mafuta.

Ofisi ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari imesema kundi la IMN limepigwa marufuku kwa sababu "limetekwa na watu wasioamni maandamano ya amani na badala yake linatumia ghasia" kufikia malengo yake.

Hii ni kufuatia mandamano ya wiki kadhaa yaliopangwa na kundi hilo kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wake Sheikh Zakzaky, ambaye amekuwa kizuizini tangu mwaka 2015, na kupigania haki ya mamia ya wafuasi wake waliouawa na vikosi vya serikali.

Baadhi ya maandamano hayo yamekubwa na makabiliano makali kati ya waandamanaji  na vikosi vya usalama,nje ya majengo ya Bunge la kitaifa.

Afisa wa polisi wa ngazi ya juu ni mmoja wa waliouawa katika mji mkuu wa, Abuja.

Kundi la IMN lilianzishwa miongo minne iliyopita na limekuwa likishinikiza kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa kidini wa Iran nchini Nigeria.

Lilichangia pakubwa mapinduzi ya Iran yaliyomsaidia Ayatollah Khomeini kuchukuwa uongozi wa taifa hilo mwaka 1979 baada ya kupinduliwa kwa utawala wa Shah uliyokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Khomeini bado inaushawishi mkubwa kwa kundi hilo: Wafuasi wa IMN kwanza walitangaza uaminifu wao kwake katika mkutano na baadae kwa kiongozi wao, Sheikh Ibraheem Zakzaky.

Kundi la IMN linajichukulia kama serikali, na Sheikh Zakzaky - ambaye amekuwa kizuizini tangu mwaka 2015 -kama chanzo kikuu cha mamlaka nchini Nigeria.

Halitambui mamlaka ya serikali ya Nigeria na linachukulia viongozi wa taifa hilo Waislamu na Wakristo kuwa mafisadi na wasiomcha Mungu.

Kundi hilo lina matawi na mfumo wa utawala katika majimbo 36 ya Nigeria hali inayoipatia sifa ya serikali.

IMN pia linaendesha shule zake na hospitali katika baadhi ya majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria yaliyo na waislamu wengi.

"Vugu vugu hili la Kiislam limesajili Wakfu unaofahamika kama Fudiyya ambao unaendesha jumla ya shule 360 za msingi na sekondari. Wakfu huo unaipunguza mzigo  serikali lakini inaashiria kuwa serikali haina uwezo wa kutoa elimu kwa watu wake," ilisema katika tuvuti yake.

Baadhi ya wanachama wake wanasadikiwa kuwa wataalamu na wasomi, huku wengine wao wakishikilia nyadhifa katika jeshi, polisi na idara ya intelijensia.

Jacob Zenn, mchambuzi wa Marekani kutoka wakfu wa Jamestown, anasema kushirikishwa kwa wanachama wa IMN katika huduma ya umma inaonyesha kwamba inasaidia "mageuzi ya Kiislam", badala ya mapinduzi, nchini Nigeria.

IMN lina umaarufu kiasi gani?

Ni kundi kubwa zaidi la Kishia nchini Nigeria. Lina uwezo wa kuvutia umati mkubwa wa watu katika mikutano yake-wakati mwingine maelfu ya watu hukusanyika katika hafal yake.

Hii ni kutokana na hatua ya Sheikh Zakzaky, ambaye alichangia kukua kwa dhehebu  hilo katika taifa lililokuwa na idadi ndogo ya Washia kabla ya mapinduzi ya Iran.

Washia wanakadiriwa kuwa kati ya 5% hadi 17% ya Waislamu ambao wanakadiriwa kuwa karibu milioni 100. Waislamu wengi nchini Nigeria ni Wasunni, sawa na wale wa Saudi Arabia au Misri.

IMN inasema ninikuhusu marufuku hiyo?

Vugu vugu la IMN limekanusha madai ya kuhusika na ghasia na kulaumu vikosi vya usalama kwa mauaji ya watu waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani .

Kundi hilo linamchukulia Rais Buhari - ambaye ni Muislamu wa dhehebu la Sunni - kama kibaraka wa Saudi Arabia, na linamshtumu kwa kutaka kuangamiza Washia nchini humo
IMN linaweza kuanza upinzani dhidi ya serikali?

Vikosi vya serikali vilishambulia makao makuu ya Boko Haram, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Maiduguri mwaka 2009,katika makabiliano yaliosababisha vifo vya zaidi ya watu 700.

Kingozi mwanzilishi wa kundi hilo, Mohammed Yusuf, alikamatwa na kuuawa katika akiwa kizuizini.

Boko Haram baadae lilifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyosababisha vifo vya watu karibu 30,000 na wengine zaidi ya milioni mbili kufurushwa makwao

Baadhi ya Wanigeria wanahofia hatua ya kupiga marufuku vugu vugu la IMN huenda ikasababisha mashambulio kama yale yamekuwa yaketekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram.

Wengine wamepuuzilia mbali uwezekano wa wanachama wa IMN ambao wengi wao ni wasomi kuanzisha vita ambavyo havitakuwa na ushindi.

BBC

Updated: 05.08.2019 15:00
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.