Mauaji ya watu yaendelea Sudan

Mauaji ya watu yaendelea Sudan

10 June 2019 Monday 08:20
Mauaji ya watu yaendelea Sudan

Khartoum, Sudan
TAKRIBAN  watu wanne wameripotiwa kuuawa katika siku ya kwanza ya mgomo wa kitaifa nchini Sudan, hii ni kwa mujibu wa madaktari wanaoegemea upande wa upinzani.

Vifo vinatokana na  vikosi vya Usalama nchini Sudan kurusha mabomu ya machozi na kutumia risasi halisi kuwatawanya waandamanaji mjini Khartoum.

Wanaharakati wameitisha maandamano ya kupinga utawala huo kuanzia Jumapili, siku kadhaa baada ya msako wa kijeshi uliyosababisha vifo vya makumi ya watu katika mji mkuu wa Khartoum.
Wafanyikazi kadhaa wa benki, uwanja wa ndege na  wa shirika la umeme nchini Sudan wamekamatwa kabla ya mgomo wa kitaifa wa kupinga utawala wa kijeshi, linadai kundi kuu la waandamanaji.

Chama cha wataalamu wa Sudan kinasema  wafanyakazi pia wanatishiwa na mamlaka nchini.

Baraza la jeshi linalotawala nchi hiyo (TMC) halijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.

Jeshi lilichukua uongozi baada ya kumg'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir mwezi Aprili, na kuahidi kurejesha utawala wa kiraia baada ya kipindi cha mpito.
Lakini wanaharakati wa kupigania demokrasia wanasema kuwa baraza la jeshi haliwezi kuaminiwa baada kuzuka kwa ghasia ambapo wafuasi wengi wa Upinzani waliuawa mjini Khartoum - na wamekata kufanya mazungumzo ya amani na viongozi wa baraza hilo.

Huku hayo yakijiri vikosi vya usalama nchini Sudan vimewakamata viongozi watatu wa upinzani baada ya kukutana na waziri mkuu wa Ethiopia mjini Khartoum ili kusaidia katika mazungumzo ya amani.

Baadhi ya maofisi na biashara zimefungwa na idadi ya magari ni chache barabarani.

Kumeripotiwa milio ya risasi huku maafisa wa usalama wakiendelea kushika doria katika baadhi ya sehemu za mji waKhartoum.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.