Meya wa Mogadishu afariki dunia

Meya wa Mogadishu afariki dunia

02 August 2019 Friday 11:50
Meya wa Mogadishu afariki dunia

Mogadishu, Somalia

MEYA wa mji wa Mogadishu nchini Somalia, Abdirahman Omar Osman amefariki dunia ikiwa ni juma moja baada ya kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga ambalo liligharimu maisha ya watu sita.

Mwanamke mmoja alijilipua ndani ya ofisi ya meya huyo wakati wa mkutano wa masuala ya usalama. Amefariki dunia mjini Doha, Qatar, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Osman ambaye alikimbilia Uingereza wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya 1990, alikuwa diwani wa London kabla ya kurejea mwaka 2008 kusaidia kuijenga upya Somalia.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab lilisema kuwa lilitekeleza shambulio hilo.

Al-Shabab ilimlenga mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, James Swan, raia wa Marekani, ambaye tayari alishaondoka kwenye jengo hilo baada ya kukutana na meya  Julai 24, 2019.

Haikujulikana ni kwa namna gani mshambuliaji huyo aliweza kuingia ndani ya ofisi hizo zilizokuwa na ulinzi mkali. Walioathirika kwenye shambulio hilo wengine ni maafisa wa juu.

Osman alitoroka Somalia mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa mkimbizi, kabla ya kupata stahada yake na uraia wa Uingereza. Pia alikuwa diwani kwa tiketi ya chama cha Labour .

Alirejea Somalia mwaka 2008, ambapo alilitumikia taifa hilo kwa nafasi ya waziri wa habari na kuwa meya wa Mogadishu mwaka 2018.

Katika ukurasa wa twitter, ujumbe wa Marekani nchini Somalia umemtaja Osman kuwa ''mshirika mzuri sana na aliyekuwa akiwatumikia raia wa Somalia bila kuchoka''.

Al-shabab inataka kuangusha utawala wa Somalia na imekuwa ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara mjini Mogadishu, pamoja na uwepo wa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Afrika na vikosi vya kijeshi vyenye mafunzo.

Kundi hili lenye mahusiano na kundi la wanamgambo wa al-Qaeda limekuwa na nguvu nchini humo.

Katika mji ambao umekuwa na makundi ya hatari, alikuwa mstari wa mbele, mpole na mwenye maadili aliyekuwa akihakikisha mambo yanakwenda.

Jina lake la utani, Mhandisi Yarisow- Mhandisi mdogo- kutokana na kimo chake, sifa zake kielimu na utendaji wake.

Kama ilivyo kwa wasomali wengi, alitoroka kwenda ng'ambo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe akaishi London kwa miongo kadhaa.

Lakini aliyaacha yote hayo na kurejea Mogadishu muongo mmoja uliopita. Ilikuwa hatua ya kijasiri sana na alijua kuwa ni yenye kuhatarisha.

Tangu wakati huo, maelfu ya watu waliokuwa wakiishi nje ya Somalia walirejea kusaidia kuijenga Somalia, iliyokuwa imekumbwa na mashambulizi ya wanamgambo wa al-Shabab.

Safari ya Somalia kuelekea kuimarika imekuwa ndefu, na bado haijakamilika.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.