Mlimbwende adai kubakwa na rais mstaafu

Mlimbwende adai kubakwa na rais mstaafu

26 June 2019 Wednesday 08:45
Mlimbwende  adai kubakwa na rais mstaafu

Dakar, Senegal

MLIMBWENDE (miss Gambia) wa zamani nchini Gambia Fatou Jallow, amesema mwaka 2015  alibakwa na rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh  wakati alipokuwa madarakani.

Ushahidi wake ni miongoni mwa ripoti ya shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch ambayo inaelezea madai mengine ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na  Jammeh.

BBC ilijaribu kuwasiliana na Jammeh ambaye kwa sasa anaishi mafichoni  nchini Equitoria Guinea , kuhusu madai hayo.
Msemaji wa chama chake cha APPR alikana madai hayo yaliotolewa dhidi ya  Jammeh.

''Sisi kama chama na raia wa Gambia tumechoka na msururu wa madai ambayo yameripotiwa dhidi ya rais wa zamani'', alisema Ousman Rambo Jatta katika taarifa iliotumwa kwa BBC.
"Rais huyo wa zamani hana muda wa kujibu uongo na kampeni za kumuharibia jina. Ni mtu anayemuogopa Mungu ambaye anaheshimu sana wanawake wa Gambia'', alisema naibu wa kiongozi wa chama hicho cha APPR.

Bi Jallow aliambia BBC alitaka kukutana na  Jammeh mwenye umri wa miaka 54 mahakamani ili ashtakiwe.

''Nimejaribu sana kuficha na kufutilia mbali habari hiyo na kuhakikisha kuwa haitakuwa moyoni mwangu. Kwa kweli sikuweza , hivyo basi nikaamua kuzungumza kwa sababu ni wakati wa kusema ukweli na kuhakikisha kuwa Yahya Jammeh anasikia kile alichokitenda.

Alisema kwamba pia yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya tume ya haki na maridhiano nchini Gambia TTR ambayo imebuniwa na rais Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi Disemba 2016.

Tume hiyo ya haki na maridhiano inachunguza ukiukaji wa haki za kibinaadamu wakati wa utawala wa miaka 22 wa Jammeh , ikiwemo ripoti za mauaji ya kiholela, ukatili na kukamatwa na kuzuiliwa kiholela.

Alilazimishwa kutoka madarakani Januari 2017 baada ya mataifa jirani kutuma vikosi vya kijeshi alipokatalia madaraka.

Bi Jallow alisema kuwa alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipokutana na Jammeh baada ya kushinda shindano la malkia wa urembo wa 2014 katika mji mkuu wa Banjul.

Miezi kadhaa baada ya kupata taji hilo, anasema kwamba rais huyo wa zamani alijifanya kama mzazi wakati alipokutana naye akimaptia ushauri, zawadi na fedha na kuandaa maji kupelekwa katika nyumba yao ya familia.

Na katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na msaidizi wa rais huyo , anasema alimuuliza iwapo wangeoana.

Alikataa wazo hilo mbali na zawadi alizokuwa akipatiwa.

Bi Jallow anasema kuwa msaidizi huyo baadaye alisisitiza kwamba anafaa kuhudhuria sherehe ya kidini katika Ikulu ya rais kama malkia wa urembo mnamo mwezi Juni 2015.

Lakini alipowasili , alipelekwa katika makao ya kibinfasi ya rais huyo.

''Ilikuwa wazi kile ambacho kingetokea'', alisema akitaja hasira ya Jammeh baada ya yeye kukataa kufunga naye ndoa.

Bi Jallow anasema alipigwa kofi na kudungwa sindano katika mkono wake.

''Alizifuta sehemu zake za siri katika uso wangu, akanisukuma nipige magoti na kunifanya vibaya''

Msichana huyo baadaye alisema kuwa alijifungia nyumbani kwao kwa siku tatu na kuamua kutorokea Senegal.

Alipokuwa mjini Dakaa mji mkuu wa Senegal , Bi Jallow alitafuta usaidizi wa mashirika kadhaa ya haki za binadaamu.

Wiki chache baadaye alipatiwa ulinzi na kupelekwa nchini Canada ambapo amekuwa akiishi tangu wakati huo.
Shirika la Human Rights Watch (HRW) na Trial International yanasema kuwa  Jammeh alikuwa na mfumo wa kunyanayasa wanawake , ambapo wanawake wengine walikua wakilipwa mshahara na serikali na kufanya kazi katika Ikulu kwa jina 'wasichana wa itifaki'', ambao walikuwa wakifanya kazi za ukarani lakini umuhimu wao mkubwa ulikuwa kushiriki ngono na rais.

BBC haikuweza kubaini madai hayo, lakini afisa mmoja wa zamani nchini humo ambaye alikubali kuzungunza bila jina lake kufichuliwa alisema kuwa anajua kuhusu mambo mabaya yaliokuwa yakitendeka katika afisi ya rais: Maafisa wa itifaki walikuwa wanawake na waliajiriwa ili kuridhisha mahitaji ya rais.

Anakumbuka kumuona bi Jallow katika Ikulu mara nyengine wakati wa usiku.

Mwanamke mwengine ambaye aliajiriwa kama afisa wa itifaki akiwa na umri wa miaka 23 alilazimishwa kushiriki ngoni na  Jammeh mwaka 2015.

Mwanamke huyo ambaye aliomba kutofichuliwa jina , alisema kuwa siku moja rais huyo alimwita chumbani mwake: alianza kunivua nguo na kusema kuwa alikuwa ananipenda , angenifanyia chochote ningetaka na familia yangu, na kwamba nisiambie mtu yeyote na iwapo nitakiuka hilo nitakiona cha mtema kuni.

''Nilihisi sina chaguo. Siku hiyo alilala nami bila kutumia kinga yoyote''.

Wengine walitaka. walihisi kuheshimiwa ama walitaka pesa, aliambia shirika la haki za kibinadamu la HRW akificha jina lake.
Alielezea vile alivyonyanyaswa kingono na rais huyo nyumbani kwake huko Kanilai, 2013 wakati alipokuwa na umnri wa miaka 22: "Jioni moja msaidizi mmoja wa rais aliniita na  kuandamana naye katika nyumba ya kibinafsi ya rais .

''Alinitaka kuvua nguo. aliniambia kwamba mimi ni msichana mdogo niliyehitaji ulinzi na alitaka kunipaka maji ya kiroho''.

Katika kisa kingine siku iliofuata, alianza kulia wakati  Jammeh alipoanza kumshika mwili wake.

Alikasirika na kumfukuza. Anasema kwamba baadaye alifutwa kazi huku ahadi ya kupata ufadhili wa masomo ikifutiliwa mbali.

Rais Barrow amesema kuwa atasubiri ripoti hiyo ya tume ya maridhiano kabla ya kuamua iwapo atamrudisha bwana Jammeh nyumbani kutoka mafichoni nchini Equitorial Guinea.

BBC

Updated: 26.06.2019 09:12
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.