Mtuhumiwa mwanaume alala gereza la wanawake

Mtuhumiwa mwanaume alala gereza la wanawake

19 June 2019 Wednesday 14:19
Mtuhumiwa mwanaume alala gereza la wanawake
Eldoret, Kenya
SINTOFAHAMU imeibuka mahakamani baada ya hakimu kuelezwa kuwa mtuhumiwa  ni mwanaume lakini alikuwa ameshikiliwa katika gereza la wanawake.

Gazeti la Daily Nation la Kenya limeripoti kuwa tukio hilo limetokea katika mahakama ya moja mjini Eldoret nchini Kenya.

Mtuhumiwa huyo  aliyetambulika kwa jina Shieys Chepkosgei siku ya Jumatatu alikamatwa katika Chuo na Hospitali ya Rufaa ya Moi alikokuwa akifanya kazi kama muuguzi mwanafunzi wa kike ingawa hakuwa amesajiliwa hapo.

Baada ya kushtakiwa, alipelekwa kwenye gereza la wanawake la Eldoret kusubiri maamuzi ya mahakama huku akitambuliwa kama mwanamke.

Hatahivyo, siku ya Jumanne askari magereza katika ukaguzi wao wa kawaida waligundua kuwa mshukiwa alikua mwanaume.

Uchunguzi wa haraka ulifanyika kubaini ukweli kabla ya kufanyiwa vipimo ili kujihakikishia jinsia yake

Hakimu wa mahakama hiyo, Charles Obulutsa siku ya Jumanne alilazimika kutoa amri nyingine ikielekeza mtuhumiwa ashikiliwe kwenye kituo cha polisi cha Eldoret Magharibi ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha jinsia yake.

Hakimu Obulutsa alichukua hatua hiyo baada ya ofisa mkuu wa gereza la wanawake la Eldoret kutaka mahakama irejee amri yake akielezea kuwa mshukiwa ashikiliwe kama mfungwa wa kiume

Katika kesi hiyo mahakama ilielezwa kuwa Juni 14, 2019 mtuhumiwa huyo akiwa na nia ya kufanya udanganyifu, alijifanya kuwa mwanafunzi wa kike wa taaluma ya uuguzi kwa jina Pamela Mulupi.

Shauri hilo litatajwa tena Juni 27, 2019.
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.