Mwanamuziki Chameleone autaka umeya jiji la kampala

Mwanamuziki Chameleone autaka umeya jiji la kampala

06 June 2019 Thursday 19:20
Mwanamuziki Chameleone autaka umeya jiji la kampala


Na mwandishi wetu

NYOTA wa muziki wa Hip hop nchini Uganda Jose Chameleone leo Juni 6, 2019 ametangaza kuingia katika medani za siasa nchini humo
Muimbaji huyo wa kibao ''Badilisha'' anaaminiwa kuwa amekuwa mfuasi wa chama tawala cha NRM, ambapo amekuwa akitumbuiza kwenye matukio ya chama hicho.

Ni kama amefuata nyayo za msanii mwenzake  Bobi Wine na kuingia katika siasa.
Bobi Wine amekuwa akikumbwa na utata wa kisiasa tangu alipogombea kiti cha ubunge mwaka 2017.
Gazeti la Uganda la Observer limemnukuu Jose Chameleone, ambaye jina lake halisi ni Joseph Mayanja kuwa  anataka kuwa Meya wa mji mkuu wa Uganda Kampala. 
Chameleone ni mmoja wa wanamuziki maarufu katika eneo la Afrika Mashariki.

Moja ya nyimbo zake zinazofahamika ni ule wa Shida za Dunia, unaozungumzia matatizo yanayowakabili watu:
Akielezea matarajio yake, amesema:"Wakati huduma zinapokuwa katika hali mbaya, watu wanaanza kuamka ...Watu wana kiu ya uongozi unaofaa na hawajaupata".

"Wale wanaodhani kuwa ni mkumbo wa Bobi Wine wana ukweli kiasi fulani ," Chameleone alinukuliwa akisema..

Bobi Wine alipiga kengele halafu akasema 'Tumekuwa watu wazima wa kutosha sasa ; Tunaweza kufanya hili '. Kwani kuna shida gani ya kufanya hilo? Kila kitu katika dunia hii kina mtu fulani aliyekianzisha ."

Chameleone anakiri kuwa ameshawishiwa na Bobi Wine. 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.