Mwili wa Mugabe waagwa

Mwili wa Mugabe waagwa

12 September 2019 Thursday 06:22
Mwili wa Mugabe waagwa

HARARE, Zimbabwe

WAZIMBABWE na wageni waalikwa takribani 100 leo Septemba 12, 2019 wataanza kutoa heshima zao za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe. Mwili wake uliwasili Septemba 11, kutokea Singapore, ambapo alifariki wiki iliyopita akiwa na miaka 95.

Mugabe, alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1980. Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi mwaka 2017.

Atazikwa siku ya Jumapili baada ya shughuli za maziko siku ya Jumamosi.

Mara baada ya kutua nchini Zimbabwe, mwili wa Mugabe ulipelekwa kwenye makazi ya familia ''Blue Roof'' mjini Harare.

Leo Alhamisi na Ijumaa, Mwili wa Mugabe utalala katika uwanja wa mpira wa Rufaro eneo la Mbare mjini Harare, ambapo ndipo alipoapishwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Zimbabwe baada ya kupatiwa uhuru kutoka kwa koloni la kiingereza mwaka 1980.

Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi ,kwenye uwanja wenye uwezo wa kupokea watu 60,000 kabla ya kuzikwa .

Rais wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa ametaja kuwa ''shujaa wa taifa'' kwa jitihada zake za kuisaidia Zimbabwe kupata uhuru wake.

Lakini ripoti zinasema kuwa Mugabe hakutaka waliomuondoa madarakani kushiriki katika maziko yake, hivyo badala yake huenda shughuli za maziko zikafanywa kwenye makazi ya familia yake.

Familia ya Mugabe inapinga mpango wa serikali wa kumzika katika makaburi ya mashujaa wa taifa katika mji mkuu wa Zimbabwe -Harare na wanataka azikwe katika kijiji alikozaliwa.

Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.

Mugabe ambaye anakumbukwa na wengi kama mkombozi ambaye aliwaondoa watu wake katika pingu za ukoloni wa wazungu walio wachache anakumbukwa na wengine kama mtu aliyeangusha uchumi wa moja ya chumi zilizotazamiwa kufanya vizuri zaid barani Afrika na ambaye aliwatesa kikatili wapinzani wake.

Alikuwa maarufu miongoni mwa wapiga kura wengi hata katika kipindi chake cha hivi karibuni alipoondolewa mamlakani.

Aliondolewa mamlakani alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye baadaye alikuwa rais wa taifa hilo.

PICHANI: Mwili wa Robert Mugabe ukifikishwa nyumbani kwake. Kushoto ni mjane wa Mugabe 

Updated: 12.09.2019 06:31
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.