Mwili wa Mugabe waagwa, kuzikwa baada ya mwezi

Mwili wa Mugabe waagwa, kuzikwa baada ya mwezi

16 September 2019 Monday 06:47
Mwili wa Mugabe waagwa, kuzikwa baada ya mwezi

HARARE, Zimbabwe

MWILI wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe umehifadhiwa katika eneo alilozaliwa mara baada ya watu kumuaga katika mji mkuu wa Harare na anatarajiwa kuzikwa baada ya mwezi mmoja. Viongozi wa Afrika wamemsifu kama mpigania Uhuru.

Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia'.

Hatahivyo uwanja ulio na uwezo wa kubeba watu 60,000 ulikuwa na idadi ndogo ya watu.

Uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.

Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira ni baadhi ya masuala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe. ''Tunafurahia kwamba amefariki, kwa nini nihudhurie mazishi yake? sina mafuta'', alisema mkazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP.

''hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. yeye ndio sababu ya matatizo yetu''.

Mazishi hayo yanafuatia mgogoro kati ya familia ya Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa.

Sasa imekubalika kwamba atazikwa katika makaburi ya mashujaa mjini Harare, familia yake imesema.

Msemaji wa familia na mpwa wake leo Mugabe anasema kwamba hiyo itafanyika baada ya kipindi cha mwezi mmoja wakati ambapo kaburi hilo litajengwa katika makaburi hayo ya mashujaa .

Kulikuwa na jua , na raia wachache walikwenda kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

Viongozi wa Afrika wa zamani na waliopo sasa waliingia katika uwanja huo kwa shangwe kubwa pamoja na viongozi waliopigania uhuru wa bara hili.

Rais Mnangagwa - mtu ambaye alimpindua Mugabe miaka miwili iliopita aliketi viti viwili karibu na mkewe Mugabe Grace.

Sifa za Mugabe kama mpiganiaji uhuru zilitolewa na kila kiongozi ambaye alisimama kuhutubia akiwemo rais wa Kenya Uhuru kenyatta - huku wakitofautiana na maneno yaliotolewa na mwakilishi wa familia hiyo Walter Chidhakwa aliyesema kwamba ''Mugabe alikuwa na huzuni , huzuni kubwa', Ilikuwa safari ngumu na ya kuchukiza''.

Matamashi yake yalionyesha wazi wasiwasi uliopo kati ya serikali iliopo na familia ya Mugabe.

Zaidi ya viongozi kumi wakiwemo wale wa zamani wa mataifa ya Afrika walihudhuria mazishi hayo , wakimsifu Mugabe kama kiongozi wa Afrika aliyeamua kutumikia maisha yake yote kwa raia wa Zimbabwe.

Rais Kenyatta alisisitiza kwamba matatizo ya Kiafrika yanahitaji suluhu ya kiafrika.

Baadae raia walimzomea rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ikionekana kuwa jibu la ghasia dhidi ya wageni nchini kwake katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Alitambua kelele hizo kwa kusema: " Katika wiki mbili zilizopita , sisi Waafrika Kusini tumekuwa tukikabiliwa na wakati mgumu.

Tumekuwa na vitengo vya ghasia katika baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini...hili limesababisha kama ninavyowasikia mkisema ... vifo na majeraha miongoni mwa idadi ya watu. lakini alisisitiza sisi Waafrika wa Kusini hatupendi ghasia dhidi ya wageni"

Updated: 16.09.2019 06:56
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.