Omar al Bashir ashtakiwa kwa ufisadi

Jeshi lilimuondoa madarakani rais huyo wa muda mrefu mwezi April, 2019 kufuatia miezi ya maandamano dhidi yake.

Omar al Bashir ashtakiwa kwa ufisadi

Jeshi lilimuondoa madarakani rais huyo wa muda mrefu mwezi April, 2019 kufuatia miezi ya maandamano dhidi yake.

14 June 2019 Friday 08:56
Omar al Bashir ashtakiwa kwa ufisadi

Khartoum, Sudan

RAIS aliyeng'olewa madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir ameshtakiwa kwa kosa la ufisadi.

Mashtaka yanahusiana na sheria zinazohusu "utajiri haramu na maagizo ya dharura ",imesema ofisi ya mwendesha mashtaka, ambayo haikutoa taarifa zaidi.

Jeshi lilimuondoa madarakani rais huyo wa muda mrefu mwezi April, 2019 kufuatia miezi ya maandamano dhidi yake.

Alhamisi Juni 13, 2019 Msemaji wa jeshi alisema  makosa yalifanyika wakati majenerali walipoamrisha kumalizika kwa mgomo wa kukaa mbele ya makao makuu ya jeshi ambapo waandamanaji wanadai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo.

Ghasia za mwezi Juni zilisababisha vifo vya watu 61, kwa mujibu wa maafisa, au 118,kwa mujibu wa madaktari wanaounga mkono waandamanaji wanaodai demokrasia.

Mazungumzo baina ya waandamanaji na baraza la kijeshi la mpito yalivunjika baada ya ghasia.

Viongozi wa baraza baadae waliyaita maandamano kuwa ni ukaidi wa raia , ambayo walisema hayana budi kukoma ili kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani.

Baada ya mkutano baina ya Tibor Nagy, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika ,na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan,jeshi lilisema kuwa lina matumaini Marekani inaweza "kuwa na mchango mzuri".

 Bashir alipinduliwa na kukamatwa Aprili  11, 2019 baada ya miongo mitatu ya utawala wa kiimla nchini Sudan. Hajawahi kuonekana kwa umma tangu alipokamatwa.

Mwezi Mei alishtakiwa kwa makosa ya kuchochea na kuhusika na mauaji ya waandamanaji.

Mashtaka hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa kuhusu kifo cha daktari aliyeuwawa wakati wa maandamano yaliyosababisha kumalizika kwa utawala wake mwezi uliopita.

Hatma ya Bashir haijawa wazi. Aliripotiwa kutiwa nguvuni mara baada ya kupinduliwa.

Mnamo mwezi Disemba, waandamanaji walianza maandamanano dhidi ya uamuzi wa serikali wa kupandisha mara tatu kwa bei ya mkate.

BBC

Updated: 14.06.2019 09:06
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.