Rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi azikwa

Rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi azikwa

18 June 2019 Tuesday 11:35
Rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi azikwa

CAIRO, Misri

RAIS wa zamani wa Misri Mohammed Morsi amezikwa leo, baada ya hapo jana kuanguka mahakamani na kuaga dunia. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yametaka kufanyika uchunguzi huru, kufahamu sababu halisi ya kifo chake.

Wakili wa rais huyo wa zamani amesema Morsi amezikwa leo asubuhi katika makaburi ya Medinat Nasr Mashariki mwa mji mkuu, familia yake ikiwepo. Televisheni ya taifa imesema kifo chake kilisababishwa na mshituko wa moyo.

Morsi, rais wa kwanza wa kiraia wa Misri, ambaye ni wa kwanza pia kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, alianguka katika kizimba chake mahakamani baada ya kujieleza, na aliwahishwa hospitalini ambako ilitangazwa kuwa alikuwa tayari amekata roho.

Tangu alipoangushwa katika mapinduzi ya kijeshi Julai 2013, aliyekuwa waziri wake wa ulinzi Abdel Fattah al-Sisi amechukua hatamu, na amefanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya maelfu ya wanachama na wafuasi wa kundi la Udugu wa Kiislam, mamia miongoni mwao wakikabiliwa na hukumu ya kifo.

Serikali ya al-Sissi yanyoshewa kidole

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Misri wamesema yumkini mazingira mabaya gerezani yamesababisha kifo cha Morsi, hali ambayo wanasema ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Mmoja wao, Amr Magdi wa shirika la Human Rights Watch amesema ''Tunaamini kwamba mazingira mabovu na ya kutengwa aliyowekwa Morsi yanakidhi vigezo vya utesaji kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa, na kanuni za msingi za hali ya wafungwa, ambazo serikali ya Misri ilizipuuza kabisa''.

Mwanaharakati huyo ameongeza kuwa anadhani serikali ya al-Sissi imeonyesha dharau ya kupindukia dhidi za haki za msingi za binadamu.

DW

Updated: 19.06.2019 09:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.