Utata waibuka kifo cha rais aliyepinduliwa Misri

Utata waibuka kifo cha rais aliyepinduliwa Misri

18 June 2019 Tuesday 06:14
Utata waibuka kifo cha rais aliyepinduliwa  Misri

Cairo, Misri
UTATA umeibuka kufuatia kifo cha  Mohamed Morsi ambaye  ni rais aliyepinduliwa madarakani mwaka 2013. Ikiwa ni mwaka mmoja tangu achaguliwe  kidemokrasia mwaka 2012 

Shirika la Amnesty International linasema kifo chake kimesababishwa na maradhi ya moyo huku kundi la Muslim Brother Hood likidai ameuwawa.

Morsi mwenye umri wa miaka 76  alifariki dunia  Juni 17, 2019 majira ya jioni mara baada ya kuanguka gafla akiwa mahakamani mchana. 

Habari zinadai pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya presha na kupanda kwa sukari mwilini.

Televisheni ya taifa ya nchi hiyo ilitangaza kuwa Morsi amefariki gafla akiwa amefikishwa mahakamani

Mohamed Morsi ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia alipinduliwa na jeshi la nchi  hiyo mwaka  2013.

Baada ya hapo amekuwa gerezani na alionekana kwa mara ya kwanza hadharani tangu kupinduliwa mwezi Julai, 2013. 

Alifikishwa mbele ya mahakama ya uhalifu ya Cairo.

Updated: 19.06.2019 09:54
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.