Wapinzani nchini Sudan wakamatwa

Wapinzani nchini Sudan wakamatwa

09 June 2019 Sunday 10:34
Wapinzani  nchini Sudan wakamatwa

VIKOSI vya usalama nchini Sudan vimewakamata viongozi watatu wa upinzani baada ya kukutana na waziri mkuu wa Ethiopia mjini Khartoum ili kusaidia katika mazungumzo ya amani.

Mohamed Ismat wa muungano wa upinzani alikamatwa siku ya ijumaa huku Imsail jalab na Mubarak Ardol wa kundi la waasi wa SPLM-North walikamatwa mapema sikju ya Jumamosi.

Hatua hiyo inajiri siku chache tu baada ya kuzuka kwa ghasia ambapo wafuasi wengi a Upinzani waliuawa.

Kukamatwa kwao pia kunajiri siku chache tu baada ya utawala wa jeshi nchini Sudan kusema kuwa uko tayari kwa mazungumzo na muunago wa upinzani.

Siku ya Ijumaa , waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alizuru taifa hilo ili kuzipatanisha pande hizo mbili ambazo alikutana nazo katika mikutano miwili tofauti.

Lakini saa chache baadaye , habari zilisambaa kuhusu kukamatwa kwa Mohamed Ismat -mwanachama wa muungano wa upinzani na afisa mkuu wa benki kuu nchini Sudan.

Baadaye wanajeshi wanadaiwa kumkamata afisa mwandamizi wa SPLM-North Ismail jalab na msemaji Mubarak Ardol. Kiongozi wa chama hicho Yasir Arman pia alikamatwa siku ya Jumatano.

Habari za kuzuiliwa kwa viongozi huo zitazua kutoaminika kwa baraza la kijeshi linalotawala. Makundi ya waandamanaji yanapanga kuendelea na kampeni yao siku ya Jumapili.

Esmat na Jalab ni viongozi wakuu wa muungano wa upinzani Freedom for Change , mwavuli wa upinzani unaoshirikisha viongozi wa maandamano na makundi ya waasi.

BBC

Updated: 09.06.2019 10:51
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.