Waziri wa fedha Kenya akana madai ya ufisadi mahakamani

Waziri wa fedha Kenya akana madai ya ufisadi mahakamani

23 July 2019 Tuesday 09:13
Waziri wa fedha Kenya akana madai ya ufisadi mahakamani

Nairobi, Kenya
WAZIRI  wa fedha nchini Kenya, Henry Rotich amekana madai ya ufisadi yaliowasilishwa mahakamani dhidi yake

Mashtaka hayo yanayohusiana na kandarasi ya ujenzi wa mabwawa mawili yamesomwa mbele yake mapema leo Julai 23, 2019

Anatuhumiwa kwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa hayo.

Rotich alikamatwa jana Julai 22, 2019. kutokana na  agizo la mkuu wa mashtaka ya umma nchini humo Noordin Haji. Honry Rotich alikamatwa pamoja na katibu mkuu wa wizara ya fedha Kamau Thuge.

Noordin amesema mashtaka dhidi ya Rotich yanatokana na uchunguzi wa polisi uliofanywa kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika mradi wa kujenga bwawa unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Italia ya CMC Di Ravenna.

Hata hivyo, Rotich amekanusha kuhusika na madai hayo na kampuni hiyo pia imeyakanusha madai hayo. Rotich ameshtakiwa pamoja na maafisa wengine kadhaa wa serikali, akiwemo katibu mkuu wa wizara ya fedha, Kamau Thugge.

Noordin Haji aliwaambia waandishi habari kwamba maafisa hao walikiuka sheria ya matumizi ya fedha za umma.

Mashtaka dhidi ya Rotich huenda yakasababisha mshtuko kwa wanasiasa wa Kenya, ambao wamezoea kupuuza kashfa za ufisadi, ambapo mara nyingi hatua zinazochukuliwa huwa ni ndogo.

Updated: 23.07.2019 12:20
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.