Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa

22 July 2019 Monday 13:38
Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa

Nairobi, Kenya

WAZIRI wa fedha nchini Kenya Henry Rotich amekamatwa. Rotich amekamatwa kufuatia agizo la mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji alilolitoa mapema leo.

Honry Rotich amekamatwa pamoja na katibu mkuu wa wizara ya fedha Kamau Thuge.

Mapema leo Julai 22, 2019 Noordin haji, alitoa agizo la kutaka waziri huyo, akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya rushwa kuhusu ujenzi wa mabwawa mawili.

Noordin amesema mashtaka dhidi ya Rotich yanatokana na uchunguzi wa polisi uliofanywa kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika mradi wa kujenga bwawa unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Italia ya CMC Di Ravenna.

Hata hivyo, Rotich amekanusha kuhusika na madai hayo na kampuni hiyo pia imeyakanusha madai hayo. Rotich atashtakiwa pamoja na maafisa wengine kadhaa wa serikali, akiwemo katibu mkuu wa wizara ya fedha, Kamau Thugge.

Noordin Haji amewaambia waandishi habari kwamba maafisa hao walikiuka sheria ya matumizi ya fedha za umma.

Mashtaka dhidi ya Rotich huenda yakasababisha mshtuko kwa wanasiasa wa Kenya, ambao wamezoea kupuuza kashfa za ufisadi, ambapo mara nyingi hatua zinazochukuliwa huwa ni ndogo.

PICHANI JUU;Waziri wa fedha nchini Kenya Henry Rotich aliyekamatwa baada ya kujisalimisha kwa tuhuma za ufisadi

DW

Updated: 23.07.2019 09:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.