Bungeni leo: Ndugulile asema hospitali zote za rufaa za mikoa sasa kupatiwa CT Scan

Alidokeza kuwa ni mpango wa serikali kuhakikisha kwamba mfumo wa upatikanaji wa mashine za CT scan unahamishiwa ngazi za hospitali za rufaa za mikoa.

30 May 2018 Wednesday 09:28
Bungeni leo: Ndugulile asema hospitali zote za rufaa za mikoa sasa kupatiwa CT Scan

Na Mwandishi Wetu

HOSPITALI zote za rufaa za mikoa sasa kupatiwa mashine maalum ya utambuzi wa magonjwa inayojulikana kam CT Scan , Naibu Waziri wa Afya, jinsi, watoto na maendeleo ya Jamii Dk Faustine Ndugulile amesema.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM) aliyetaka kujua sababu zinazosababisha serikali kuchelewa kupeleka mashine hizo kwenye hospitali ya mkoa kama Sekou Toure iliyopo jijini Mwanza.

Naibu Waziri Ndugulile alisema kuwa tatizo la ukosefu wa CT scanner kwenye hospitali ya Sekou toure litakwisha mwishoni mwa mwaka huu.

Alisema kuwa serikali ipo katika maongezi na Netherland wa kuangalia namna ya kupatiwa mashine hiyo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Alidokeza kuwa ni mpango wa serikali kuhakikisha kwamba mfumo wa upatikanaji wa mashine za CT scan unahamishiwa ngazi za hospitali za rufaa za mikoa.

Kwa sasa alisema wizara ya afya inafanya mahitaji ya mashine hizo katika hospitali za rufaa za mikoa nchini Tanzania.

Akijibu swali lingine lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Zawadi Koshima (CCM) aliyetaka kujua lini mashine ya CT itapelekwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Bugando, Naibu Waziri huyo alisema serikali ipo katika hatua za kusambaza mashine hizo.

Alisema kwa hospitali hiyo tayari imekwisha pelekewa mashine na kufungwa rasmi kuanzia mwezi Januari mwaka huu, na kuahidi kuitafutia mashine ya MRI.

Azania Post

Updated: 30.05.2018 11:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.