Jaffo anusa ufisadi wa kutisha hospitali ya Sinza Palestina

Kituo kinahudumia watu wengi sana lakini bado hakijakidhi hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya

Jaffo anusa ufisadi wa kutisha hospitali ya Sinza Palestina

Kituo kinahudumia watu wengi sana lakini bado hakijakidhi hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya

01 June 2018 Friday 12:04
Jaffo anusa ufisadi wa kutisha hospitali ya Sinza Palestina

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jaffo amesema kuwa hajaridhika na kiasi cha fedha kinachokusanywa kwenye kituo cha afya cha Sinza Palestina kilichopo Dar es Salaam.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Suzan Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) aliyetaka kujua sababu za serikali kutokipatia fedha za kutosha kituo hicho na kuongeza eneo lake ili kuwezesha wananchi wengi kupata huduma.

Waziri Jafo alisema kuwa ni kweli kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali na hivi karibuni alikitembelea kwa lengo la kuangalia thamani halisi ya pesa.

Alisema kuwa aligundua kituo kinahudumia watu wengi sana lakini bado hakijakidhi hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya.

Alidokeza kuwa pamoja na wingi wa watu wanaotembelea eneo hilo, lakini mapato yanayopatika hakuridhika kwani hayalingani na idadi ya wagonjwa.

Alisema kuwa serikali ina mpango wa kujenga hospitali za wilatya tatu katika mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka huu wa fedha.

Akijibu maswali ya wabunge Damas Ndumbaro Songea mjini (CCM), Desderious Mipata (Nkasi) na Abdallah Chikota Nanyamba (CCM), Waziri Jaffo alisema kuwa serikali ina mpango wa kujenga hospitali za wilaya 67 nchi nzima.

Alisema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 105 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hizo Tanzania nzima.

Alisema yale maeneo ambayo hayata bahatika kujengewa hospitali za aina hiyo, serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya watahakikisha kuwa angalau wanapata huduma za vituo vya afya.

Kuhusu ajira za watumishi wa afya, Jafo alisema kuwa serikali imetoa kibali kwa ajira 6,180 na itahakikisha sekta hiyo inapata watendaji.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.