JKCI yaanza kutibu maeneo yanayopitisha umeme kwa wingi moyoni

JKCI yaanza kutibu maeneo yanayopitisha umeme kwa wingi moyoni

02 August 2019 Friday 11:15
JKCI yaanza kutibu maeneo yanayopitisha umeme kwa wingi moyoni

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanza kuziba maeneo  yanayopitisha umeme kwa wingi na kuleta shida katika moyo kwa kutumia mashine maalum (Electrophysiology machine)

Vilevile wagonjwa 10 wenye matatizo ya umeme wa moyo ambao mapigo yao  yanadunda  haraka kuliko kawaida na wengine yako chini ya asilimia 30 wamefanyiwa matibabu na taasisi hiyo.

Wamefanyiwa matibabu hayo na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa shirika la madaktari wa Marekani .

Akizungumza  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Dk Peter Kisenge amesema kati ya wagonjwa 10 waliofanyiwa upasuaji, wanne mioyo yao ilikuwa imechoka na mapigo ya moyo kuwa chini ya asilimia 30 wamewekewa kifaa maalum cha kuongeza utendaji kazi wa moyo  kijulikanacho kwa jina la kitaalamu la 'Cardiac Resynchronization Therapy implantable cardioverter Defibrillator'(CRTD).

Dk Kisenge aliongeza "Kwa mara ya kwanza JKCI imeanza kuziba maeneo ambayo yanapitisha umeme wa moyo kwa wingi na kuleta shida katika moyo kwa kutumia mashine maalum (Electrophysiology machine) iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya matibabu ya moyo  nchini''.

“Mashine hii ya Electrophysiology inakazi ya kupima umeme wa moyo kama kuna mahali ambapo unapita bila kufuata njia ya kawaida pataonekana na baada ya hapo inatumika  kuziba njia hizo. Tatizo hili huwatokea zaidi wagonjwa wenye shinikizo la juu la moyo la  muda mrefu, wagonjwa wanaopata mshituko wa moyo, na wagonjwa wenye hitilafu ya umeme wa moyo katika  baadhi ya vyumba vya moyo,” amesema Dk Kisenge.

Daktari huyo amesema  matibabu ya kuziba maeneo yanayopitisha umeme wa moyo bila kufuata njia yake  awali hayakuwepo nchini na kupelekea wagonjwa wenye shida hiyo kupelekwa nje ya nchi lakini kuanzia Julai 22 mwaka huu matibabu hayo yameanza kutolewa.

Naye Mtaalamu wa mashine ya kuchunguza, kutathmini na kutibu umeme wa moyo unaoenda kwa haraka (Electrophysiologist) kutoka Shirika la Madaktari Afrika la Nchini Marekani Prof. Mathew Sachest amesema Madaktari Afrika wamekuwa wakishirikiana na madaktari wa JKCI kwa kipindi cha miaka mitatu sasa ambapo utoaji wa huduma za matibabu ya moyo umekuwa  kwa kasi ya hali ya juu hivyo kupunguza uhitaji wa wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Prof. Sachest amesema kupitia kambi maalum za matibabu wanazozifanya JKCI  madaktari , wauguzi na mafundi sanifu wa moyo wanapata  uzoefu wa kutoa huduma za matibabu zinazohitaji ujuzi wa hali ya juu na kuweza kutoa huduma hizo kwa wagonjwa.

Updated: 02.08.2019 11:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.