Mikoa tisa kupata mashine za kusafisha figo

Mikoa tisa kupata mashine za kusafisha figo

17 June 2019 Monday 15:06
Mikoa tisa kupata mashine za kusafisha figo

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

SERIKALI imesema mikoa tisa itapewa mashine mpya za kupima na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.

Mikoa hiyo ni  Tanga, Mwanza, Kigoma, Kagera, Arusha, Iringa, Mtwara, Unguja na Zanzibar, hali itayosaidia kupunguza gharama kwa kuwasogezea wagonjwa huduma hizo.

Hatua hiyo ni kufuatia  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupokea mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo na itazisambaza katika Hospitali za rufaa  kote nchini.

Uamuzi huo umetangazwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  leo Juni 17, 2019 jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea mashine hizo zenye thamani ya bilioni 1.55 kutoka kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief wakiongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini.

Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kusambaza na kuboresha huduma hizi na kwa sasa zinapatikana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi.

"Sisi kama Serikali tumeendelea kuboresha hizi huduma, kwa sasahivi zinapatikana Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi" alisema Dkt. Ndugulile 

Amesema Serikali inaendelea kuboresha huduma hizo licha ya kuwepo changamoto ya idadi kubwa ya wahitaji wa huduma na kwamba Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mashine 42 

Pia naibu waziri huyo  amesema katika kipindi cha miaka mitatu Serikali imefanikiwa kupunguza magonjwa yakuambukiza kwa asilimia 50 na kuwa changamoto kubwa ipo  katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ambukiza ya kisukari, presha na figo ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mitindo ya maisha.

"Timepiga hatua kubwa sana katika magonjwa yakuambukiza, ambayo tumeyapunguza kwa asilimia 50 ndani ya miaka mitatu, tumepunguza vifo na maambukizi ya Malaria, lakini tumepunguza vile vile maambukizi ya Ukimwi, sasa changamoto inayotukabili ni magonjwa yasiyo yakuambukiza kama, kisukari, presha na magonjwa ya figo,"amesema Dkt Ndugulile. 

Akiongea kwa niaba ya kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Naibu Balozi wa Saudia Arabia nchini Ahmed Bin Saleh Alghamdi ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada inayoendelea kuchukua katika kutatua changamoto kwenye Sekta ya Afya na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo baina ya nchi hizo mbili.

Updated: 17.06.2019 15:26
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.