Muhimbili yapokea shehena ya madawa kutibu majeruhi ajali ya moto

Muhimbili yapokea shehena ya madawa kutibu majeruhi ajali ya moto

14 August 2019 Wednesday 14:03
Muhimbili yapokea shehena ya madawa kutibu majeruhi ajali ya moto

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili(MNH) imepokea dawa na vifaa tiba  kutoka Bohari ya Dawa (MSD) zitakazotumika kuwahudumia majeruhi wa ajali ya moto waliohamishiwa hospitalini hapo kutoka mkoani Morogoro.

Agosti 10, 2019 eneo la Msamvu Morogoro lori la mafuta lilianguka na kusababisha mlipuko ambapo hadi sasa watu zaidi 80 wamefariki dunia

Makabidhiano haya ya dawa yamefanyika leo Agosti 14 jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwitikio wa maombi ya dharura yaliyoombwa na Hospitali Muhimbili kwa ajili na majeruhi hao.

Meneja wa MSD, Kanda ya Dar es Salaam Celestine Haule amesema mpaka sasa jumla ya shehena tano zimekabidhiwa hospitalini hapo Muhimbili zikiwemo dawa muhimu.

Updated: 14.08.2019 14:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.