NIMR yafafanua dawa ya kutibu saratani ya tezi dume.

NIMR yafafanua dawa ya kutibu saratani ya tezi dume.

15 July 2019 Monday 14:57
NIMR yafafanua dawa ya kutibu saratani ya tezi dume.

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa ya uwepo wa dawa ya mitishamba ya kutibu saratani ya tezi dume

Taarifa ya leo Julai 15, 2019 ya NIMR inaeleza; 

Kutokana na uzito wa suala hili na kuzingatia mateso ya wagonjwa wenye tezi dume NIMR ingependa kufafanua na kurekebisha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Ni kweli kwamba moja ya dawa za miti-shamba ambazo NIMR imetengeneza imeonesha dalili ya kupunguza uvimbe kwa wagonjwa wenye tatizo la kuvimba tezi dume. 

Dawa hii haijaonesha uwezo wa kutibu saratani ya tezi dume. Dawa hii bado iko katika hatua ya uchunguzi wa kitafiti.  Lengo letu la kushiriki katika maonesho ya Sabasaba lilikuwa ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya.

Baadaye kama tafiti hizo zitakuwa na matokeo mazuri zinaweza kutumika baada ya kufuata hatua za kisheria za usajili. 

Tunaomba radhi kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na ripoti hiyo iliyokuwa inasambaa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.