Sakata mtoto kukatwa kiganja, Waziri atoa wiki mbili

Sakata mtoto kukatwa kiganja, Waziri atoa wiki mbili

12 September 2019 Thursday 13:34
Sakata mtoto kukatwa kiganja, Waziri atoa wiki mbili

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa wiki mbili kwa Baraza la Madaktari Tanganyika na Baraza la Wauguzi kuchunguza suala la mtoto kukatwa kiganja kilichoharibika baada ya kuchomwa sindano kupitia mshipa

Waziri huyo amesema, watu wamekuwa wakitibiwa kienyeji katika vituo vya kutolewa huduma kutokana na huduma za maabara kutofanya vizuri

Mtoto huyo wa miezi mitano, amekatwa kiganja baada ya kupatiwa huduma ya matibabu ya sindano kupitia mshipa wa mkononi na kupelekea mkono huo kuharibika na kukatwa kabisa

Matibabu hayo yalifanyika katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dar es Salaam na baadae alipewa rufaa kwenda hospitali ya taifa ya Muhimbili(MNH) baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na mkono ukizidi kubadilika rangi na kuwa mweusi huku ukisinyaa

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.