Serikali kutoa muongozo kudhibiti Dengue

Serikali kutoa muongozo kudhibiti Dengue

19 June 2019 Wednesday 10:17
Serikali kutoa muongozo kudhibiti Dengue


Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imesema itatoa maelekezo maalumu ya dawa zinazopaswa kutumika kuangamiza viruiruia vinavyosababisha ugonjwa wa Dengue.

Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa tishio la kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo hasa jijini Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu leo Juni 19, 2019 Bungeni  jijini Dodoma amesema baada ya siku tatu serikali itatoa muongozo wa matumizi ya dawa zitakazotumika kuangamiza  wadudu (Mbu) wanaoeneza ugonjwa huo.

"Ugonjwa wa Dengue unaambukizwa na Mbu baada ya siku tatu serikali itatoa muongozo wa  jinsi ya kudhibiti vuruirui vya Mbu vinavyosabisha ugonjwa huu,'' amesema

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ilala(CCM),Mussa Zungu aliyeitaka serikali kutoa dawa za chenga na kuzigawa kwa wananchi bure ili kuangamiza mazalia na kuuwa vidudu vivyosababisha ugonjwa wa Dengue. 

Updated: 19.06.2019 10:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.