‘Wachangiaji damu watakiwa kutoa taarifa sahihi za afya zao’

‘Wachangiaji damu watakiwa kutoa taarifa sahihi za afya zao’

15 August 2019 Thursday 11:42
‘Wachangiaji damu watakiwa kutoa taarifa sahihi za afya zao’

Na mwandishi wetu, Mbeya

WACHANGIAJI Damu nchini wametakiwa kutoa taarifa sahihi kuhusu hali zao za kiafya na kwamba wengi wanadaganya.

“Hivi sasa wengi wa wanaochangia damu hawatoi kwa usahihi taarifa za afya zao. Tunabaini damu haifai mara baada ya kuifanyia vipimo. Kitendo ambacho ni hatari kwa afya za wanaohitaji kuongezewa damu,’’ amesema Ofisa Uhusiano na Ustawi wa Jamii wa Damu Salama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Charton Meena

Akizungumza na Azaniapost leo Agosti 15, 2019 amesema kufuatia hali hiyo kanda hiyo inatarajia kubadilisha utaratibu ili kudhibiti hali hiyo.

‘'Hadi kujua damu kuwa ipo salama ni lazima uipime mara nne. Unapoipima mara moja inaweza isikupe majibu sahihi,’’ amesema

Wakati huo huo Meena amesema kwa kipindi cha Juni 2018 hadi Julai 2019 katika Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, mkoa wa Mbeya unaongoza kwa uchangiaji damu salama, imetoa lita 8,682 ukifuatiwa na Ruvuma lita 6,889, Rukwa lita 5,306, Songwe lita 5,282, Iringa lita 4,482 na Njombe lita 3,287.

"Kimsingi hali ya uchangiaji ni ya kuridhisha kwa kipindi cha Juni na Julai mwaka huu kiwango kimeongeza kutoka asilimia 66 hadi 70 jumla ya wananchi 2,836 wamechangia kutoka katika taasisi, vyuo na shule za sekondari. Kwa mwaka takribani watu 48,994 ujitokeza kuchangia damu kwa hiari, "amesema.

Pamoja na mambo mengine ameitaka jamii kuendelea kuchangia damu kwa hiari ili kuweza kusaidia wagonjwa wenye uhitaji hususan wanaofanyiwa upasuaji, wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, upungufu wa damu ,ajari za moto, barabarani na wanaopandikizwa figo ili kuokoa maisha yao.

Updated: 15.08.2019 11:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.