Wajue viumbe watatu wanaosababisha vifo vingi kwa binadamu

Mbu anasababisha vifo kati ya milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.

Wajue viumbe watatu wanaosababisha vifo vingi kwa binadamu

Mbu anasababisha vifo kati ya milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.

27 May 2019 Monday 11:08
Wajue viumbe watatu wanaosababisha vifo vingi kwa binadamu
Simba, Nyati, Faru, Chatu....haya ndiyo majina ya VIUMBE yanayoweza kukujia akilini pindi ukiulizwa KIUMBE YUPI NI HATARI ZAIDI KWA MWANADAMU. Amini usiamini, kiumbe hatari zaidi ni mdogo mara elfu kadhaa akilinganishwa kiumbo na hao majabali tunaowafahamu. Na udogo wake si katika umbile pekee bali pia hata sauti yake ni ndogo kulinganisha na mbwa, paka au mbuzi, achilia mbali wababe kama Simba, Chui au Faru. Kiumbe huyo hatari wa kuogopwa kwa gharama yoyote ile ni MBU.

Ifuatayo ni viumbe watatu wanaosababisha vifo vingi vya binadamu hada sasa:

(1) MBU

Kwa mujibu wa takwimu, Mbu ni kiumbe hatari zaidi kuliko wote duniani. Kiumbe huyo hatari ni maarufu kwa kuambukiza rundo la magonjwa, kubwa zaidi ikiwa ni homa ya malaria. Lakini pia mbu hueneza homa ya matende (elephantiasis), homa ya manjano (yellow fever), kindiga popo (dengue fever) na homa ya Mto Nile.

Mbu anawajibika kusababisha kati ya vifo milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.

MAKAZI: Takriban dunia nzima lakini zaidi barani Afrika, Asia na Amerika ya Kaskazini.

ANAVYOSABABISHA MAAFA: Mbu huambukiza maradhi kwa kuuma kwenye ngozi ya binadamu na kumwaga mate yake yenye vijidudu vinavyosababisha homa husika.


Ukiweka kando vipele vidogo vinavyotokea mahala alipouma mbu, anayeambukizwa na mbu hatambua maambukizo hadi pale kinga za mwili inaposhuka (na kuleta dalili mbalimbali).

JINSI YA KUMKWEPA: Njia ya kupambana na mbu na maambukizo ni pamoja na  kutumia chandarua kilichomwagiwa kinga, kuangamiza sehemu za mazalio ya mbu na vidonge vya kinga.

(2) NYOKA WENYE SUMU KALI
Kuna zaidi ya aina 2,000 za nyoka, kati yao wenye sumu ni 450 na ni  250 tu kati yao ndio wenye uwezo wa kuua binadamu.

 Nyoka wenye sumu kali husababisha kati ya vifo 50,000 na 250,000 kwa mwaka.

MAKAZI: Zaidi ni Afrika, Asia na Amerika ya Kaskazini

WANAVYOSABABISHA MAAFA: Nyoka wana kasi sana na sehemu yoyote katika mwili wa binadamu inawezwa  kugongwa na kiumbe huyo hatari. Lakini ni hatari zaidi nyoka anapomgonga mtu kwenye mshipa wa damu kwani  huarakisha kusambaa kwa sumu ya kiumbe huyo. Nyoka hutumia sumu yao kumlegeza mtu na pengine kumpotezea fahamu.


Majoka makubwa kama Mfalme Kobra (King Cobra) yanaweza kusimama hadi usawa wa kichwa cha binadamu,huku wengine wakiweza kutema na kurusha sumu yao kutoka mbali kwenda kwenye macho ya mwanadamu.

JINSI YA KUWAKWEPA: Mara  nyingi nyoka hushambulia pale tu pale anapobughudhiwa.


Ushauri muhimu wa kuepuka shambulizi kutoka kwa viumbe hao ni kujiepusha nao.

Pia ni muhimu kuvaa mabuti kwenye mazingira yanayoweza kuwa na nyoka.Epuka mapori yanayoweza kuwa makazi ya nyoka.

Na ikitokea umeomwona nyoka,inashauriwa urudi kinyumenyume taratibu kwani anaweza kujirusha mara nusu ya urefu wake,na mtikisiko kidogo tu unaweza kuamsha hasira za kiumbe huyo hatari.

(3) NG'E


Ni kiumbe hatari mwenye sura mbaya maradufu.Inaaminika kuwa ng'e anasababisha vifo vingi zaidi ya vile vinavyorekodiwa rasmi, sababu ni mazingira wanayoishi viumbe hao na ugumu wa kupatikana tiba dhidi ya sumu yao.

Hata hivyo, kuna aina tofauti 1500 za ng'e na ni 25 tu kati yao  ndio hatari kwa uhai wa  binadamu.

Ng'e husababisha kati ya vifo 800 hadi 2,00 kwa mwaka

MAKAZI: Duniani kote hususan Afrika,America ya Kusini na Kaskazini na Asia ya Kati.

WANAVYOSABABISHA MAAFA: Ng'e humlegeza binadamu baada ya kumdunga sumu kwa kutumia "vijisindano" vilivyopo kwenye mikia yao.Kama ilivyo kwa sumu nyingine za wadudu/wanyama,binadamu walio hatarini zaidi ni wale wenye aleji,japo ng'e wengi wenye sumu wanaopatikana Afrika wanaweza kumdhuru mtu yeyote yule.

JINSI YA KUWAKWEPA: Ng'e huwa 'active' zaidi nyakati za usiku na hupendelea kupumzika mchana. Ni muhimu kuhakikisha sehemu ya kulala ipo salama kabla ya kuubwaga mwili. Kadhalika ni muhimu kukung'uta mavazi au soksi kuhakikisha hakuna ng'e humo,vinginevyo itakuwa balaa.

Updated: 27.05.2019 11:19
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.