Baraza kuu la usalama la UN lapiga kura dhidi ya kitendo cha Israel

Azimio hilo pia limelaani kurushwa kwa maroketi kutoka Ukanda wa Gaza hadi maeneo ya raia nchini Israel, lakini halikutaja jina la Hamas, kundi lenye msimamo...

Baraza kuu la usalama la UN lapiga kura dhidi ya kitendo cha Israel

Azimio hilo pia limelaani kurushwa kwa maroketi kutoka Ukanda wa Gaza hadi maeneo ya raia nchini Israel, lakini halikutaja jina la Hamas, kundi lenye msimamo...

14 June 2018 Thursday 11:27
Baraza kuu la usalama la UN lapiga  kura dhidi ya kitendo cha Israel

Na Mwandishi Wetu

UMOJA wa Mataifa kupitia baraza la usalama umepiga kura dhidi ya kitendo cha Israel kutumia nguzu za ziada kuzima ghasia na maandamano jirani na mpaka baina yake na Ukande wa Gaza .

Iliripotiwa kuwa Nchi 120 kati ya 193 wanachama zimeunga mkono azimio hilo ambalo pia limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupendekeza mkakati wa kimataifa wa kuyalinda maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kimabavu na Israel. Kura nane tu ndizo zililipinga azimio hilo, na nchi 45 zilijizuia kupiga kura.

Azimio hilo lilifikishwa katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa na Algeria, Uturuki na Wapalestina, baada ya Marekani kulizuia kwa kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapema mwezi huu.

Azimio hilo pia limelaani kurushwa kwa maroketi kutoka Ukanda wa Gaza hadi maeneo ya raia nchini Israel, lakini halikutaja jina la Hamas, kundi lenye msimamo mkali wa Kiislamu linalotawala katika Ukanda wa Gaza. Ingawa maazimio yanayopitishwa katika baraza kuu hayana uzito kisheria, yana umuhimu mkubwa kisiasa.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amelikosoa azimio hilo akisema linaegemea upande mmoja, kwa kutolitaja kundi la Hamas ambalo amesema ndilo chanzo cha vurugu katika Ukanda wa Gaza. Marekani ilijaribu kulifanyia marekebisho azimio hilo kwa kuingiza kundi la Hamas, lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

Marekebisho hayo yaliungwa mkono na nchi 62, yakapingwa na nchi 58, huku nyingine 42 zikichagua kutopiga kura kabisa.

Naye balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon, amedai kuwa kwa kupitisha azimio hilo, baraza hilo kuu la Umoja wa Mataifa limeonyesha kula njama na kundi la kigaidi.

Muakilishi wa Wapalestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour amesema wanachokihitaji ni ulinzi wa raia wao, na kutoa hoja kwamba kupitishwa kwa azimio hilo kutasaidia kupunguza mivutano.Mansour amesema na hapa namnukuu, ''Hatuwezi kusalia kimya tukikabiliwa na uhalifu mkubwa unaotumia ghasia na kuvunja haki za binadamu za watu wetu'', mwisho wa kumnukuu.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.