Bodi wakurugenzi CRDB yatupia mbali maombi ya wanahisa kuhusu Dk Kimei

Baadhi ya mafanikio ya Dk Kimei tangu alipojiunga na Benki mwaka 1998 ni kuimarika sana; na kuwa kinara katika ubunifu wa bidhaa na huduma katika soko pamoja...

Bodi wakurugenzi CRDB yatupia mbali maombi ya wanahisa kuhusu Dk Kimei

Baadhi ya mafanikio ya Dk Kimei tangu alipojiunga na Benki mwaka 1998 ni kuimarika sana; na kuwa kinara katika ubunifu wa bidhaa na huduma katika soko pamoja...

07 June 2018 Thursday 09:26
Bodi wakurugenzi CRDB yatupia mbali  maombi ya wanahisa kuhusu Dk Kimei

Na Mwandishi Wetu

MAOMBI ya baadhi ya wanahisa wa Benki ya CRDB kuhusu Mkurugenzi Mtendaji wake Dk Charles Kimei kuendelea na wadhifa huo baada ya kuwa muda wake umemalizika yamekataliwa.

Taarifa iliyotolewa leo na kusainiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo Ally Laay na pia Dk Kimei imesema kuwa mchakato wa kumpata mrithi wake utaendelea kama kawaida.

Hivi karibuni baadhi ya wanahisa wa benki hiyo wakiwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka jijini Arusha walipendekeza Dk Kimei aendelee na wadhifa wake.

Mwishoni mwa mwaka jana benki hiyo ilitoa taarifa ya kuanza rasmi kwa mchakato wa kumpata mrithi wa Dk Kimei, kufuatia kukaribia kwa muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria mwanzoni mwa mwaka 2019.

Kufuatia taarifa hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Benki iliunda kamati maalum itakayorasimu zoezi hilo na kuwa mchakato huo ulioanza mwezi Januari 2018 na unatarajia kukamilika mnamo mwezi Januari 2019.

Dk Kimei ambaye amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB tangu mwaka 1998, ataendelea na nafasi hiyo mpaka tarehe 31 Mei 2019.

Baadhi ya mafanikio ya Dk Kimei tangu alipojiunga na Benki mwaka 1998 ni kuimarika sana; na kuwa kinara katika ubunifu wa bidhaa na huduma katika soko pamoja na kuifanya kuwa Benki chaguo nambari moja kwa watanzania.

Mengine ni funguaji wa kampuni tanzu nchini Burundi (CRDB Bank Burundi Ltd) pamoja na kampuni tanzu za CRDB Bank Microfinance Ltd na CRDB Bank Insurance Ltd ambazo zote zinafanyakazi chini ya mwamvuli wa kampuni mama ya CRDB Bank PLC.

Katika kipindi chake cha uongozi kama Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya CRDB imefanikwa kupiga hatua kubwa ikiwemo kukua kwa faida kutoka shilingi bilioni 2 mwaka 1998 hadi kufikia shilingi bilioni 108 mwaka 2016, huku rasilimali za Benki zikikua kutoka shilingi bilioni 54 hadi kufikia shilingi trilioni 5.3 mwaka 2016. Pia mtandao wa matawi umekua kutoka matawi 19 mwaka 1998 hadi matawi 262 mwaka 2017.

Azania Post

Updated: 07.06.2018 15:47
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.