Bungeni Leo: Mwinyi sasa kumaliza migogoro ya mipaka baina ya jeshi na wananchi nchi nzima

Alikuwa akijbu swali la nyongeza la Mbunge wa Morogoro mjini , Abdulaziz Abood (CCM) aliyetaka kujua lini wananchi wa kata za Kauzeni na Luhongo watarudishwa...

Bungeni Leo: Mwinyi sasa kumaliza migogoro ya mipaka baina ya jeshi na wananchi nchi nzima

Alikuwa akijbu swali la nyongeza la Mbunge wa Morogoro mjini , Abdulaziz Abood (CCM) aliyetaka kujua lini wananchi wa kata za Kauzeni na Luhongo watarudishwa...

30 May 2018 Wednesday 11:34
Bungeni Leo: Mwinyi sasa kumaliza migogoro ya mipaka  baina ya jeshi na wananchi nchi nzima

Na Mwandishi Wetu

MIGOGORO ya mipaka kati ya jeshi la ulinzi na wananchi huenda inaweza ikawa historia mara baada ya serikali kuonyesha dhamira ya dhati kutatua changamoto hiyo ya muda mrefu nchini Tanzania, bunge limeambiwa.

Akizungumza leo katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Hussein Mwinyi alisema kuwa amekwisha andaa tayari utaratibu wa kutatua changamoto hiyo.

Alikuwa akijbu swali la nyongeza la Mbunge wa Morogoro mjini , Abdulaziz Abood (CCM) aliyetaka kujua lini wananchi wa kata za Kauzeni na Luhongo watarudishwa maeneo yao yaliyochukuliwa na jeshi.

Waziri Mwinyi alisema kuwa jeshi halina migogoro ya kimipaka na kata za Kauzeni na Luhogo kwani maeneo hayo yalipimwa na yapo kimkakati na haitokuwa vyema kwa jeshi kuondoka.

Hata hivyo alisema kuwa migogoro ya mipaka baina na Jeshi na wananchi ipo katika maeneo mengi nchini na sasa yupo tayari kwenda na watalaam wake kuyapatia ufumbuzi wa kudumu ili kuleta amani.

Mbali ya Morogoro alitaja changamoto nyingine ya mipaka kuwa inapatikana kule katika jimbo la Kyela lililopo chini ya waziri wa habari, michezo , Utamaduni na sanaa Dk Harrison Mwakyembe.

“Najua kule kwa Mwakyembe maeneo ya Kajunjumele , bondeni kuna changamoto ya mipaka kote nitafika kutatua ,” alisema Waziri Mwinyi.

Aidha aliwataka wananchi wote waliovamia kambi za kijeshi kwa kujenga nyumba zao kuondoka mara moja.

Updated: 30.05.2018 12:23
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.