Kamati ya bajeti yarudisha hoja tano kwa Spika, 19 zakubaliwa

Akifafanua alisema kuwa ilionekana kuwa Wizara ya elimu ilipata fedha nyingi wakati asilimia kubwa ya bajeti hiyo itakwenda kwenye bodi ya mikopo.Alisema...

Kamati ya bajeti yarudisha hoja tano kwa Spika, 19 zakubaliwa

Akifafanua alisema kuwa ilionekana kuwa Wizara ya elimu ilipata fedha nyingi wakati asilimia kubwa ya bajeti hiyo itakwenda kwenye bodi ya mikopo.Alisema...

14 June 2018 Thursday 11:07
Kamati ya bajeti yarudisha hoja tano kwa Spika, 19 zakubaliwa

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Bunge ya bajeti imesema kuwa illipokea hoja 24 za serikali ambapo 19 zilifikiwa muafaka na tano ambazo zinatakiwa kujadiliwa zaidi walizirejesha kwa Spika .

Akizungumza asubuhi hii kwenye mahojiano mwenyekiti wa kamati hiyo Hawa Ghasia alisema kuwa walikuwa na mashauriano na serikali huko mkoani Dodoma kuanzia tarehe 11 hadi jana

Alizaja hoja hizo kuwa ni ile inayohusu mfuko wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, walimu wa sayansi, ushuru wa korosho zinazosafirishwa nje, fedha za ruzuku isiyokuwa na masharti na vitendea kazi vya idara ya zimamoto.

Akifafanua alisema kuwa ilionekana kuwa Wizara ya elimu ilipata fedha nyingi wakati asilimia kubwa ya bajeti hiyo itakwenda kwenye bodi ya mikopo.Alisema kuwa kamati ilipendekeza kuwa fedha hizo zigawanywe na kupelekwa kwa matumizi ya kawaida.

Kuhusu walimu wa sayansi, mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa nchi ina upungufu wa watendaji 15,000 .

Alisema kuwa kamati iliomba ajira na fedha zitengwe lakini serikali ikasema kuwa kiasi kilichopo kinatosheleza na mchanganuo ukaonyesha kuwa walimu elfu nne tu waliotakiwa kuajiriwa lakini kmati ilikataa na kuomba 15, 000 waajiriwe.

Ghasia alisema hoja ya ushuru wa korosho ililetwa na kiti ( mwenyewe) kwa fedha hazikupelekwa kwenye mfuko wa pembejeo matokeo yake bei ikapanda sana.

Alisema kuwa zao hli lilifanya vizuri sana mwaka jana na serikali inatakiwa kulilea kwani kwa sasa zaidi ya mikoa 17 inalima Alidokeza kuwa endapo bodi ya Korosho ingetekeleza vizuri mipango yake ya miaka kumi , Tanzania ingekuwa nchi ya kwanza duniani kwa uzalishaji wa zao hilo.

Alisema kuwa hoja ya fedha ya ruzuku isiyokuwa na masharti inayotolewa na serikali kuu na kwamba walikubaliana kuwa serikali itoe shilingi bilioni 251.

Baada ya majadiliano serikali iliahdi kutoa shilingi bilioni 68 na kiasi kilichobaki kutolewa kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

Alisema kuwa katika ruzuku hiyo halmashauri zinajipangia miradi mikubwa miwili au mitatu ambayo italeta manufaaa makubwa kwa jamii.Alibainisha kuwa wameridha na ahadi za serikali lakini wameitaka ihakikishe zinatekelezwa.

Kuhusu idara ya zimamoto alisema kuwa ina upungufu mkubwa wa magari kwani kwa sasa yapo 19 tu nchi nzima. Alisema baada ya tathmini Wizara ya fedha imeagiza idara hiyo kuendelea na mchakato wake wa kununua magari.Aliongeza kuwa serikali itatoa fedha lakini inatakiwa suala hilo walipe kipaumbele sana kwani kwa sasa kuna majengo mengi marefu na ya kisasa.

Hata hivyo alidai kuwa bajeti ya mwaka huu itasaidia kukuza uchumi kwani imetengeneza mazingira wezeshi na kuongeza kipato kwa wananchi wa kawa

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.