Kitendo cha Merkel kutetea wahamiaji haramu kinaweza kuiangusha serikali yake?

Seehofer ambaye yuko kwenye mgogoro wa wazi na Kansela Angela Merkel, mgogoro ambao unatishia hali ya utulivu na masikizano katika serikali ya muungano...

Kitendo cha Merkel kutetea wahamiaji haramu kinaweza kuiangusha serikali yake?

Seehofer ambaye yuko kwenye mgogoro wa wazi na Kansela Angela Merkel, mgogoro ambao unatishia hali ya utulivu na masikizano katika serikali ya muungano...

14 June 2018 Thursday 11:12
Kitendo cha Merkel kutetea wahamiaji  haramu kinaweza kuiangusha serikali yake?

Na Mwandishi wetu

KANSELA Angela Merkel anakabiliwa na wakati mgumu kuhusu sera yake ya wakimbizi inayotishia kuiporomosha serikali yake ya mseto.

Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer ambaye yuko kwenye mvutano mkubwa na Kansela Merkel kuhusu suala la wakimbizi amesema yeye na wenzake wa Italia na Austria, Matteo Salvini na Herbert Kicki wameunda ushirikiano wiki hii kukabiliana na wahamiaji haramu, mpango ambao unapingwa na Kansela Merkel.

Mawaziri wa mambo ya ndani wenye msimamo mkali kutoka Austria, Ujerumani na Italia wameunda ushirikiano maalum wa kukabiliana na wahamiaji haramu, hilo ni tangazo alilolitoa Kansela wa Austria Sebastian Kurz mjini Berlin, tamko ambalo linauzidisha mvutano uliotanuka barani ulaya kuhusu suala la wahamiaji.

Tamko hilo la Kurz limekuja baada ya kukutana na waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer na linatowa ujumbe mahsusi kwa kansela Angela Merkel ambaye anajaribu kutafuta ushirikiano wa nchi za Umoja wa Ulaya kuhusu mahali pa kuwapeleka wanaotafuta hifadhi.

Seehofer ambaye yuko kwenye mgogoro wa wazi na Kansela Angela Merkel, mgogoro ambao unatishia hali ya utulivu na masikizano katika serikali ya muungano nchini Ujerumani anasema ushirikiano wake pamoja na mawaziri wenzake wa ndani wa Italia na Austria utakwenda mbali zaidi na kuyaangalia masuala ya usalama na ugaidi ingawa hakutowa maelezo ya kina kuhusu jinsi lengo hilo litakavyotimizwa.

"Jana nilizungumza na waziri wa mambo ya ndani wa Italia kwa simu na akasema kwamba anatamani kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya Rome, Vienna na Berlin, katika ngazi ya mawaziri kukabiliana na masuala kama usalama, ugaidi na uhamiaji, na mimi niliridhia.''

Kansela Merkel ameupinga kwa nguvu zote mpango uliopendekezwa na waziri wake wa mambo ya ndani Seehofer wa kuwarudisha wahamiaji ambao wameshajiandikisha katika nchi nyingine ya Umoja wa Ulaya, wanaofika katika mipaka ya Ujerumani wakitaka kuomba kuingia nchini kuomba hifadhi.

Merkel anasema Ujerumani haipaswi kuchukua uamuzi kivyake wakati ambapo Ulaya inatafuta sera ya pamoja kuhusu suala la wahamiaji. Awali alipotembelea klabu ya soka ya SV Rot-Weiss Victoria Mitte mjini Berlin, Merkel alitoa mfano wa jinsi watu wanavyoishi kwa kusema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.