banner68

Ugonjwa mpya unaoambukizwa kwa ngono waibuka

Wataalamu wa afya waonya, waanza kuwa sugu kwa dawa

Ugonjwa mpya unaoambukizwa kwa ngono waibuka

Wataalamu wa afya waonya, waanza kuwa sugu kwa dawa

11 July 2018 Wednesday 09:44
Ugonjwa mpya unaoambukizwa kwa ngono waibuka

Ugonjwa ambao unafahamika kidogo unaweza kuwa ni mbaya zaidi iwapo watu wataacha kuwa waangalifu zaidi, wataalamu wanaonya.

Mycoplasma genitalium (MG) kama unavyofahamika kitaalamu mara nyingi hauna dalili lakini unaweza kusababisha maumivu ya tumbo la chini, na kuwaacha baadhi ya wanawake tasa.

MG inaweza ikakosewa – na iwapo haitatibiwa inavyopasa, inaweza kusababisha usugu dhidi ya dawa za antibiotic.

Chama cha Afya ya Ngono na Ukimwi nchini Uingereza kinatoa ushauri mpya. Kimeandaa mwongozo wa namna ya kutibu MG.

MG ni nini?

Mycoplasma genitalium ni bakteria ambaye anaweza kusababisha maumivu ya ureta kwa wanaume, na kusababisha kutokwa na maji maji kwenye uume na kusababisha maumivu wakati wa kukojoa.

Kwa wanawake, unaweza kusababisha maumivu ya via vya uzazi, yaani mji na mirija ya uzazi, kusababisha maumivu na homa na kutokwa na damu.

Unaweza kuupata kwa kufanya mapenzi bila kinga na mtu ambaye anaugonjwa huo. Kondomu zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi zaidi.

MG mara nyingi haina dalili na sio wakati wote unahitaji matibabu, lakini unaweza kukosewa au kudhaniwa kuwa ni ugonjwa mwingine wa kingono, mfano Klamidia.

Vipimo vya MG vimetengenezwa hivi karibuni lakini havipatikani kila mahali japokuwa madaktari wanaweza kupeleka sampo za wagonjwa katika sehemu vipimo vinapatikana ili kupata majibu.

Unaweza kutibiwa kwa antibiotic – lakini ugonjwa huo umeanza kuwa sugu kwa dawa hizo.

Kila mmoja anaweza kujilinda na ugonjwa wowote unaoambukizwa kwa ngono kwa matumizi sahihi ya kondomu na wapenzi wapya na wale wasio rasmi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.