banner58

Viogozi wa kitaifa wanamsubiri Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa ASDPII asubuhi hii

Lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima..

Viogozi wa kitaifa wanamsubiri Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa ASDPII asubuhi hii

Lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima..

04 June 2018 Monday 09:19
Viogozi wa kitaifa wanamsubiri Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa ASDPII asubuhi hii

Na Mwandishi Wetu

VIONGOZI i wakuu wa kitaifa tayari wamekwisha wasili kwenye tukio la uzinduzi wa program ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDPII) unaofanyika asubuhi hii jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaonyesha kuwa viongozi waliowasili eneo la tukio kwenye ukumbi w Kimataifa wa Julius Nyerere ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baadhi ya mawaziri, makatibu wakuu na watendaji kutoka sekta binafsi

Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba, mgeni rasmi kwenye sherehe za leo ni Rais John Magufuli.

Dkt Tizeba alisema, Wizara za kisekta zikijumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ndizo zenye jukumu la kuhakikisha ASDP II inakuwa na mafanikio makubwa nchini na kuwa mkombozi wa wananchi katika kilimo.

Alisema kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa miaka kumi (10) kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ambapo kipindi cha kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24.

Lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi; kuongeza pato la Taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na lishe.

Aidha, Programu hii itatekeleza sera mbalimbali kama vile Sera ya Kilimo ya Taifa, Sera ya Mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa Chakula na Lishe, Sera ya Ugatuaji Madaraka, Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sera ya Mashirikiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi.

Azania post itaendelea kukuletea taarifa zaidi la tukio hili muhimu kwa ajili ya Tanzania, tafadhali ubaki kwenye mtandao

Azania Post

Updated: 04.06.2018 11:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.