Vita kati ya bodaboda, askari usalama barabarani imekwisha,asema mwenyekiti

Alisema kuwa kwa sasa waendesha bodaboda wengi wa wilaya hiyo wamekuwa na urafiki na askari wa usalama barabarani baada ya kukubali kufuata sheria zote

07 June 2018 Thursday 09:49
Vita kati ya bodaboda, askari usalama barabarani imekwisha,asema mwenyekiti

Vita kati ya bodaboda, askari usalama barabarani imekwisha,asema mwenyekiti

Na Mwandishi Wetu

DHANA ya uadui kati ya waendesha pikipiki na askari wa usalama wa barabarani haipo tena kutokana na elimu inayoendelea kutolewa imefahamika.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda na Bajaj wa wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania Almano Mdede alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu sekta hiyo ya usafirishaji.

Alisema kuwa kwa sasa waendesha bodaboda wengi wa wilaya hiyo wamekuwa na urafiki na askari wa usalama barabarani baada ya kukubali kufuata sheria zote.

“Hakuna tena vita kati ya bodaboda na polisi, hapo awali madereva wengi walikuwa hawajiamini na wengi walikuwa hawajakamilika, lakini kwa sasa sababu hizo hakuna tena wamebaki kuwa marafiki”, alisema.

Alipongeza jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa kuendelea kuwaelimisha waendesha pikipiki hao kuhusu sheria na kanuni za usalama.

Kuhusu kupungua kwa ajali kulikokuwa kunasababishwa na unywaji wa pombe ya viroba, alisema kuwa siyo kweli kwamba madereva wote walikuwa wanatumia.

Alisema kupungua kwa ajali hakutokani na kupigwa marufuku kwa unywaji wa viroba, bali ni elimu ambayo imekuwa ikitolewa na jeshi la polisi.

Aliwashauri waendesha pikipiki hao kuwa wasafi na kuendelea kufanya kazi yao kwa weledi kwani ni ina heshima na kuweza kuwabadilisha maisha kama wataitumia vizuri.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.