banner68

Ajabu: Liko wapi kaburi la Saddam Hussein?

Mtu aliyeitawala Iraki kwa mkono wa chuma kwa kiasi cha robo karne alinyongwa alfajiri ya Desemba 30, 2006

Ajabu: Liko wapi kaburi la Saddam Hussein?

Mtu aliyeitawala Iraki kwa mkono wa chuma kwa kiasi cha robo karne alinyongwa alfajiri ya Desemba 30, 2006

16 April 2018 Monday 13:49
Ajabu: Liko wapi kaburi la Saddam Hussein?

Katika kijiji alikozaliwa wa Al-Awjah, kaburi mahsusi la dikteta wa Iraq aliyeuawa kwa kunyongwa Saddam Hussein limeharibiwa vibaya kwa kuvunjwa huku uzio unalozunguka eneo hilo ukiwa umeondolewa na kukiwa hakuna hata alama ya mabaki ya mwili wake.

Mtu aliyeitawala Iraki kwa mkono wa chuma kwa kiasi cha robo karne alinyongwa alfajiri ya Desemba 30, 2006, na kuzusha shangwe kwa waislamu wa madhehebu ya Shia ambao kwa miaka mingi walikuwa wakionewa na wale wachache wa madhehebu ya Suni.

Rais wa Marekani George W. Bush binafsi aliwahi kutoa amri ya uhamisho ya haraka ya mwili wa dikteta huyo kwa kutumia helikopta ya kijeshi ya jeshi la Marekani kutoka Baghdad kwenda mji wa kaskazini ya Tikrit, karibu na Al-Awjah.

Lakini leo hii, siri na mashaka imetanda juu ya ni wapi alipozikwa mtu ambaye jina lake kwa miaka mingi lilivijaza vichwa vya Wairaqi kwa hofu. Je! Mwili wake bado uko katika Al-Awjah au ulikuwa umehamishwa, na kama ni hivyo, ulipelekwa wapi?

Kaburi la Saddam Hussein limeharibiwa sana. [Picha na AFP]


Sheikh Manaf Ali al-Nida, kiongozi wa kabila la Albu Nasser ambalo ukoo wa Saddam unatokea, kwa muda mrefu ameshikilia barua ambayo familia yake ilitia saini wakati ilipopokea mwili, na kukubali kwamba Saddam atazikwa haraka bila kuchelewa.

Saddam, mwenye umri wa miaka 69, alipumzishwa kabla ya alfajiri katika kaburi alilotengeneza mwenyewe miaka kadhaa nyuma. Eneo hilo limegeuka kuwa sehemu iliyotembelewa sana na wafuasi na makundi ya wanafunzi wa kutoka eneo hilo ambao hutembelea katika siku za kuzaliwa kwa Hussein, Aprili 28.

Leo, wageni wanahitaji idhini maalum ya kuingia eneo hilo, eneo ambalo limeharibiwa kabisa, na Sheikh Nida amelazimika kuondoka kijijini hapo na kwenda kutafuta kimbilio katika eneo la Wakurdi ya Iraq.

Tangu baada ya uvamizi ulioongozwa na Marekani wa mwaka 2003, kabila lake wamekuwa "wanatuonea kwa sababu sisi tulikuwa karibuna Saddam", alisema, amevaa nguo za jadi za keffiyeh kichwani ambayo ni mavazi ya makabila ya Iraki.

"Je, ni kawaida kwamba tunapaswa kulipa gharama kubwa kiasi hicho kwa kizazi baada ya kizazi tu kwa sababu sisi ni wa familia moja?"

‘Limelipuliwa’ katika kaburi Saddam, wanamgambo hasa wa Kishia wa muungano wa Heshi al-Shaab, walikabidhiwa kazi ya usalama katika eneo hilo, wanasema kaburi liliharibiwa kufuatia shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Iraki baada ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la Islamic State kuweka walenga shabaha (snipers) katika paa za kaburi hilo.

Sheikh Nida hakuwapo kwa kushuhudia mlipuko huo - lakini anaamini kuwa kaburi la Saddam "limefunguliwa na kulipuliwa".

Jaafar al-Gharawi, mkuu wa usalama wa Hashed, alisisitiza: "Mwili bado uko hapo." Moja ya wapiganaji wake, hata hivyo, anadhani kwamba binti wa Saddam anayeitwa Hala anayeishi uhamishoni aliwasili katika eneo hilo kwa kutumia ndege binafsi na kuondoka na mwili wa baba yake hadi nchini Jordan.

"Haiwezekani!" alisema profesa wa chuo kikuu na mwanafunzi wa muda mrefu wa zama za Saddam, ambaye alikataa kutoa jina lake.

"Hala hajarudi tena Iraki," alisema.

"(Mwili), unaweza kuwa amechukuliwa mahali pa siri… hakuna anayefahamu nani ameutoa na ameupeleka wapi.”

Ikiwa ndivyo ilivyo, familia ya Saddam ingekuwa imelinda kwa karibu sana siri juu ya eneo hilo, aliongeza.

Kaburi la Saddam lingeweza kukutana na hali ile ile kama ile ya baba yake, katika mlango wa kuingia kijijini, ambapo palilipuliwa kwa bomu. Lakini wengine, ikiwa ni pamoja na mkazi wa Baghdad Abu Samer, wanaamini kuwa Saddam bado yuko hai mahali fulani.

"Saddam haikufa," alisema.

"Ilikuwa ni mmoja ya watu wanaofanana nae ambaye alinyongwa."

Azania Post

Updated: 16.04.2018 16:32
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.