Anyongwa na wananchi kwa kumuua, na kuchinja mwili wa mpenzi wake

Alipanga kutorosha mwili wake kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi

Anyongwa na wananchi kwa kumuua, na kuchinja mwili wa mpenzi wake

Alipanga kutorosha mwili wake kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi

14 June 2018 Thursday 17:04
Anyongwa na wananchi kwa kumuua, na kuchinja mwili wa mpenzi wake

Mshtuko uliwakumba wakazi mji wa Kisumu nchini Kenya siku ya Alhamisi asubuhi baada ya mtu aliyekuwa akijaribu kutoa mwili wa mtu kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi alipopigwa na kunyongwa na kundi la watu wenye hasira.

Wakazi mji huo waliamka mapema asubuhi na kukutana na mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa vipande vipande, ukiaminika kuwa ni wa msichana anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 19 na kuwekwa kwenye begi.

Mita chache kutoka kwenye eneo hilo la kutisha ni nyumba ya mwanaume huyo ambaye ameishi kwa muda mfupi, kulikuwa na mwili mwingine ukiwa katikati ya bwawa la damu.

Watu waliojawa na hasira walimpiga mwanaume huyo hadi kifo chake.

Mtu huyo, Mike Otieno, 47 anasemekana alikuwa na mwanamke huyo aliyejulikana kama Achieng katika klabu moja ya usiku huko Kondele siku ya Jumatano usiku kabla ya kurudi naye nyumbani majira ya saa nane alfajiri.

Mashuhuda walisema mtu huyo alikuwa alinyongwa alfajiri ya Alhamisi baada ya mlinzi wa usiku walipotoa taarifa juu ya jaribio lake la kuutoa mwili wa mpenzi wake kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi.

"Mlinzi alisema alisikia kilio kikali cha kuomba msaada kutoka kwenye nyumba ya mwanaume huyo kabla ya vilio hivyo kumezwa na sauti kubwa ya muziki muda wa saa kumi na nusu alfajiri," alisema Mkuu wa Kituo Kikuu cha polisi cha Kisumu, Meshack Kiptum.

Alisema, mlinzi huyo alishtuka mnamo muda wa saa 10 alfajiri mwanaume huyo alipomwomba afungue geti ili rafiki zake waingie na kumsaidia kuhamisha mzigo muhimu.

Hata hivyo mlinzi alijawa hofu baada ya kumwona mwanaume huyo akisafisha damu ndani ya nyumba yake.

Mama mwenye nyumba, Margaret Nyarangi alisema mlinzi aliyejawa woga alimpa taarifa juu ya yale aliyoyaona.

"Mara moja nilikwenda kituo cha polisi cha Kondele kutoa taarifa na kurudi na maafisa wawili.

"Wakati polisi walipofika, alijaribu kukimbia kwa kutumia mlango wa nyuma ambapo watazamaji wachache walikusanyika lakini ndipo alipokamatwa na kupigwa hadi kifo chake," alisema.

Mtu huyo, mama huyo aliendelea, alikuwa amekaa kwenye nyumba hiyo kwa siku tisa tu.

Nyumba hiyo, aliongeza, ilitafutwa na kusajiliwa na mwanamke tofauti ambaye walihamia pamoja. Lakini mwanamke huyo alitoweka.

"Mwanamke ambaye alikuja kutafuta nyumba kupitia wakala wangu alisema anamiliki biashara ya vipodozi mjini. Lakini walihamia pamoja na bado hawakuweka nyaraka zao kwa wakala, "alisema, akiongeza kuwa mwanamke huyo hakuonekana tena.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.