Askari wauwa kwa bomu la kutegwa, Kamishna wa Polisi athibitisha

Ni katika mji wa mpakani baina ya Kenya na Somalia

Askari wauwa kwa bomu la kutegwa, Kamishna wa Polisi athibitisha

Ni katika mji wa mpakani baina ya Kenya na Somalia

06 June 2018 Wednesday 18:22
Askari wauwa kwa bomu la kutegwa, Kamishna wa Polisi athibitisha

Na Mwandishi Wetu

BOMU limewaua askari watano nchini Kenya katika mji uliompakani na Somalia, taarifa zimeleeza.

Imearifiwa kuwa askari hao wameuawa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara katika mji wa mpaka kati ya nchi hiyo na Somalia mapema leo.

Kamishna wa polisi wa kaunti ya Kirinyaga Joshua Chepchieng amethibitisha tukio hilo, akisema askari polisi hao walikuwa wakielekea kwenye kituo cha mpakani cha Liboi wakati gari lao lilipokanyaga bomu hilo.

Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.