Augustine Mrema amuibukia Diamond Platnumz, anena mazito

Mrema alikuwa anazungumza na redio ya Times FM

Augustine Mrema amuibukia Diamond Platnumz, anena mazito

Mrema alikuwa anazungumza na redio ya Times FM

08 June 2018 Friday 12:06
Augustine Mrema amuibukia Diamond Platnumz, anena mazito

Na Mwandishi Wetu

Kama ulikuwa hujui viongozi wa kisiasa nao wanapenda burudani tena ya muziki wa Bongo Flava kama tulivyoona kwa wanasiasa vijana kama Zito Kabwe, Hamis Kigwangala na Esta Bulaya wakizisifia kazi mbalimbali za wasanii wa muziki huo.

Habari ikufikie kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amesema msanii wa Bongo Flava anayemfuatilia kwa sana ni Diamond Platnumz.

Ni msanii ambaye anafanya vizuri anakonga roho yake pindi anapomsikia akiimba huku akichagizwa na kujituma kwake kimuziki. Mrema ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na kituo cha Times FM kuwa endapo atapewa ushirikiano, basi msanii huyo nyota atafika mbali sana.

“Namfuatilia sana Diamond, ni kijana mdogo, muimbaji mahiri. Yaani Diamond asaidiwe naona hatima yake katika maisha yake na nchi yetu atatufikisha mahali pazuri. Kwa muziki wake unakosha roho, hata sisi wazee, mimi naridhika sana,” Mrema ameiambia Times FM.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa serikali kuwa karibu zaidi na wasanii, hata hivyo amesema anaziona jitihada za Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe za kukutana na wasanii kila mara hasa pale wanapopata matatizo na kuwasaidia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
taus athumani 2018-09-12 21:14:30

ranadhani hamid