Bajeti ya 2018/2019: Pato la Taifa lazidi kuongezeka

Bajeti ya 2018/2019: Pato la Taifa lazidi kuongezeka

14 June 2018 Thursday 19:54
Bajeti ya 2018/2019: Pato la Taifa lazidi kuongezeka

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema kuwa pato la taifa limeongezeka kutoka shilingi trilioni 47.1 mwaka 2016 mpaka Shilingi trilioni 50.5 kwa mwaka 2017.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akieleza mwenendo wa uchumi kwa mwaka 2017 huku akibainisha kuwa pato la kila mwananchi limeongezeka.

“Kutokana na kuimarika kwa pato la taifa, hata pato la mtu mmoja mmoja nalo limeimarika na pato la kila mwananchi limeongezeka kutoka Shilingi milioni 2.1 mwaka 2016 mpaka Shilingi milioni 2.3 kwa mwaka,” amesema Dk Mpango.

Hata hivyo, Dk Mpango amesema kuwa sekta zilizochangia kuimarika kwa pato hilo ni uchimbaji madini na mawe iliyokua kwa asilimia 17.5, uchukuzi na usafirishaji mizigo asilimia 16.6 na habari na mawasiliano asilimia 14.7.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.