Bemba kula Idd el fitri na familia yake kwa muda

ICC imemwachia kwa muda Bemba, baada ya kumuondolea hatia wiki iliyopita

Bemba kula Idd el fitri na familia yake kwa muda

ICC imemwachia kwa muda Bemba, baada ya kumuondolea hatia wiki iliyopita

13 June 2018 Wednesday 16:52
Bemba kula Idd el fitri na familia yake kwa muda

Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) imemruhusu aliyekuwa kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Pierre Bemba kwenda nyumbani kwake kwa muda ambapo ataitwa tena mwezi ujao.

Taarifa zinasema kuwa ICC imemwachia kwa muda Bemba, baada ya kumuondolea hatia wiki iliyopita.

Kuachiwa huko kwa muda kunafungamana na tuhuma za kuwahonga mashahidi wakati kesi yake ilipokuwa ikisikilizwa mwaka uliopita, ambayo kesi yake ya rufaa itasikilizwa tarehe 4 mwezi ujao wa Julai.

Majaji wa mahakama ya ICC walimruhusu kuondoka katika jela ya mahakama hiyo mjini The Hague, ikiwa ataheshimu masharti magumu aliyowekewa.

Mojawapo ya masharti hayo ni kuripoti mara moja kwenye vyombo vinavyohusika akitakiwa kufanya hivyo, kutobadilisha anuani yake bila kuiarifu mahakama, na kujizuia kutoa tangazo lolote hadharani.

Wakili wa Bemba Peter Haynes amesema mteja wake ananuia kurejea mjini Brussels kujiunga na familia yake iliyoko huko.

Azania Post

Keywords:
ICC
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.