banner68
banner58

Bungeni Leo: Mbunge CCM aihoji serikali kuhusu ahadi ya kuwasaidia vijana kiuchumi

Aidha Majaliwa alidokeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ina kitengo mala cha kuhakikisha kuwa vijana wanaongezewa ujuzi na kutoa mwito kuhakikisha kuwa wanashiriki..

Bungeni Leo: Mbunge CCM aihoji serikali kuhusu ahadi ya kuwasaidia vijana kiuchumi

Aidha Majaliwa alidokeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ina kitengo mala cha kuhakikisha kuwa vijana wanaongezewa ujuzi na kutoa mwito kuhakikisha kuwa wanashiriki..

17 May 2018 Thursday 11:06
Bungeni Leo: Mbunge CCM aihoji serikali kuhusu ahadi ya kuwasaidia vijana kiuchumi

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalum Amina Mollel(CCM) ameihoji serikali kuhusu ahadi yake ya kuwasaidia vijana kupata maeneo ya kufanya shughuli zao.

Alikuwa akiuliza swali kwa Waziri Mkuu ambapo alisema kuwa vijana ndio nguvu ya taifa na kuitaka serikali kueleza imefikia wapi katika kuwasaidia.

Akijibu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , alisema kuwa ni kweli serikali ina mpango wa kuendelea makundi mbali mbali wakiwemo vijana. Alisema kuwa tayari imetoa mwelekeo kwa wakuu wa mikoa na wilaya na wameka maazimo ya kuandaa fursa ili vijana wafanye kazi zitakazowaingizia kipato.Alisema kuwa kila mkoa unatakiwa kutenga maeneo wkwa ajili ya kuwapa fursa makundi mbali mbali ya kijamii kufanya kazi zao..

Aidha Majaliwa alidokeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ina kitengo mala cha kuhakikisha kuwa vijana wanaongezewa ujuzi na kutoa mwito kuhakikisha kuwa wanashiriki vizuri.

Aliwataka pia kutumia vizuri miongozo mbali mbali inayotolewa ili waendelee kufanya vizuri na pia wazee nao.

Akijibu swali lingine la Mbunge wa Magu Desdery Kiswaga (CCM) aliyetaka kujua kama ipo tayari kuwachukulia hatua waharibifu wa miundombinu mbali mbali , Majaliwa alisema kuwa haitasita kufanya hivyo.

Waziri Mkuu alisema serikali inatumia fedha nyingi sana kwa ajili ya ujenzi wa barabara , majengo na miundombinu mengine na kuongeza kuwa jukumu la kuilinda ni letu sote.

Alisema kuwa ikitokea mtu mmoja anaharibu miundombinu hiyo serikali haiwezi kukaa kimya na kuongeza kuwa kila mtanzania ana dhamana ya kuilinda.

Akitolea mfano alisema hivi karibu mtu mmoja alikamatwa mkoani Shinyanga akiiba miundombinu ya barabara na kuomba kuikemea tabia kama hiyo.

Alisema kuwa anaamini uongozi wa mkoa utakuwa umemchukulia hatua kali mhusika huyo .

Aliwashauri watanzania kuendelea kuilinda miundombinu hiyo , kuwakamata waharibifu na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria.

Azania Post

Updated: 17.05.2018 11:49
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.