banner68
banner58

Bungeni leo: Tupo tayari kuunga mkono Uyui ikibadilisha jina-Waziri

Alisema kuwa kama kuja fedha ambazo zimekosea kupelekwa kwenye halmashauri husika lazima zirudishwe mara moja.

Bungeni leo: Tupo tayari kuunga mkono Uyui ikibadilisha jina-Waziri

Alisema kuwa kama kuja fedha ambazo zimekosea kupelekwa kwenye halmashauri husika lazima zirudishwe mara moja.

14 May 2018 Monday 11:27
Bungeni leo: Tupo tayari kuunga mkono Uyui ikibadilisha jina-Waziri

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali imesema kuwa haina shaka na uamuzi wa wilaya ya Tabora kubadilisha jina na kuitwa Uyui, Naibu Waziri Joseph Kakunda ameliambia Bunge leo asubuhi Jijini Dodoma

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Kaskazini , Almas Maige(CCM) aliyetaka kujua lini jimbo hilo litabadilishwa jina na kuitwa Uyui na kama wizara ipo tayari kuwaunga mkono.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Kakunda, alisema kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapendekezo ya kubadili jina la Jimbo yanatakiwa kuwasilishwa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kufuata taratibu zote zinazotakiwa

Kuhusu mkanganyiko wa jina la Halmashauri ya Tabora na manispaa ya Tabora , Naibu Waziri Kakunda alizitaka mamlaka zilizofanya makosa kuyarekebisha mara moja.

Alisema kuwa kama kuja fedha ambazo zimekosea kupelekwa kwenye halmashauri husika lazima zirudishwe mara moja.

Akijibu swali lingine kuhusiana na upungufu wa walimu wa sayansi katika shule za msingi nchini lililoulizwa na Mbunge wa Magu Boniventura Kiswaga (CCM) , Naibu Waziri Kakunda alisema kuwa serikali imeanza kutatua tatizo hilo.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ina upungufu wa walimu wa sayansi wapatao 19,000 ambapo mwaka huu wataajiri 6,000.Alidokeza kuwa nia ya serikali ni kuondokana kabisa na tatizo la upungufu wa walimu katika shule zote ifikapo mwaka 2021.

Kuhusu upungufu wa walimu Jimbo la Magu, alisema wataajiriwa kulingana na mahitaji wanayopelekwa na halmashauri husika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Imani Mwakajoka 2018-05-14 22:58:52

Tumewasoma Wazee Wa Kiki Mmeona Tumekaribia Patamu 2020