Changamoto za maendeleo Tanzania zaainishwa

"Sera ya Elimu inaongoza hususan mjadala ambao umeshindikana hadi leo juu ya kutumia Kiswahili badala ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote"

Changamoto za maendeleo Tanzania zaainishwa

"Sera ya Elimu inaongoza hususan mjadala ambao umeshindikana hadi leo juu ya kutumia Kiswahili badala ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote"

28 May 2019 Tuesday 11:50
Changamoto za maendeleo Tanzania zaainishwa

 
FELIX KAIZA
MAENEO matatu yenye  changamoto za maendeleo nchini Tanzania yaliainishwa wakati wa afla ya chakula  cha Futari iliyoandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI) jijini Dar es Salaam wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sera ya Elimu ilichomoza  wakati waalikwa walipogusia hoja kubwa na nyingi ambazo zimetolewa kuhusiana na matumizi ya Kiswahili na Kiingereza kama njia ya kufundishia. 

Ilitambulika kuwa ingawa watunga sera wa Afrika ya baada ya mkoloni hawataki kamwe kusikia habari za ubora wa elimu inayotolewa katika lugha ya kigeni, ukweli huu unajitokeza wazi kwenye sera zao. 

Kama Ngugi wa Thiong'o, katika kitabu chake cha  Decolonizing the Mind  anavyosema: “Kuchagua lugha na jinsi itakavyotumika ni suala la msingi kuhusiana na watu wanavyojielezea kulingana na mazingira yao asilia na kijamii na kweli kabisa kuhusiana na ulimwengu mzima kwa ujumla.”

Katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (1969) Tanzania ilisema   kuwa nafasi ya Kiingereza itachukuliwa na Kiswahili katika kutoa elimuya sekondari  na baadaye katika ngazi ya elimu ya juu. Sera hii haikutekelezwa.    

Katika mwaka 1982 ripoti ya Tume ya Rais kuhusu Elimu ilibainisha wanafunzi kukosa ufasaha wa Kiingereza na Kiswahili na kupendekeza mabadiliko katika lugha ya kufunidishia kwa kutumia Kiswahili katika ngazi zote za chini mwaka 1985 na hatimaye kufikia kwenye ngazi ya vyuo vikuu 1992.  

Ushauri huu wa wanazuoni ulikataliwa na Serikali pamoja na Chama Tawala.  Kiingereza kikabaki kuwa lugha ya kufundishia kwenye shule za sekondari na taasisi za elimu ya juu.

Hafla ilitambua kuamka kwa ari ya kusoma vitabu hususan miongoni mwa vijana na kupendekeza uainishaji wa watunzi wa vitabu katika lugha zote mbili sambamba na kuweka juhudi katika kufungua maktaba shuleni na vijijini.  

Sekta nyingine iliyojitokeza ilikuwa ya mipango miji.  Ukakosolewa utaratibu wa kuchagua mahali pa kujenga makao makuu mapya ya mikoa na wilaya  pembezoni mwa miji ambayo imekwisha endelezwa badala  ya mahali ambapo itakuwa kitovu cha kuleta maendeleo katika eneo husika. 

Ulitolewa mfano wa makao makuu ya Wilaya ya Kisarawe  ambayo yanaonekana kuwa zaidi sehemu pembezoni mwa Jiji la Dar es salaam. Hapo hapo, makao makuu ya Mkoa wa Pwani yamejengwa Kibaha kilometa chacke tu nje ya Dar es Salaam. 

Mwenyeji wa hafla hiyo, Rais wa KDI Ali Akkiz, alisema ujengaji wa namna hii ni changamoto ya dunia nzima. Upo mtindo wa kujenga ili wakazi wafuate na pale ambapo wapanga miji wanafuata kwenye nyayo za wakazi, ambayo huleta changamoto nyingi.  

Hapa ndipo afla ikapendekeza kutilia maanani  suala la kuhifadhi mazingira. Jiji la Dar es Salaam lilionekana kama eneo linalohitaji kufikiriwa kwa ukaribu zaidi hususan kutokana na mafuriko ya kila mwaka ya Jangwani.  Kwa nini usibuniwe utaratibu wa kuvuna maji haya, kuyasafisha na kuyasambaza kwa watumiaji?

Wakati huo huo inasemekana kwa kutokana na takwimu za ukuaji miji, Jiji la Dar es Salaam litashika nafasi ya tatu kwa wingi wa watu katika Bara la Afrika,  baada ya  Lagos ya Nigeria  na Kinshasa ya Zaire.

Updated: 03.06.2019 09:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.